KAMATI NA KAZI ZAKE
Uongozi wa Kundi
Wafuatao ni Viongozi Waanzilishi wa Kundi ambao wamekuwepo toka kuanzishwa kwa Kundi mwaka 2010 hadi sasa;
- Martin Kessy kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Arusha…. Mwenyekiti
- Ignace Massao kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma ….Makamu Mwenyekiti
- Anna Jensen Msowoya kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam…..Katibu Mkuu
- Josephine Kajembe kutoka Jimbo la Dar es Salaam -Katibu Msadizi
- Salome Ng’ingo kutoka jimbo la Dar es Salaam – Katibu Msadizi
- Catherine Patrick kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam…..Mweka Hazina
- Prosper Magali kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam….. Msemaji wa Kundi na Kiongozi wa Shughuli za Kijamii
- Majegero Selecius na Nicolaus Mtakingilwa kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam…… Wasimamizi na Waongozaji Kundi Mtandaoni (Group Admins/Directors)
Walezi wa Kundi
Baba Benno Kikudo kutoka Parokia ya Kibaha, Jimbo Kuu la Dar es Salaam amechaguliwa Mlezi Mkuu akisaidiana na Baba Timothy Maganga wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Huruma, Mbezi Beach, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Sababu za Mababa hawa kupendekezwa kuwa Walezi ni pamoja na
- Wanapatikana mara kwa mara kwenye mitandao
- Wanafahamu mengi kuhusu mitandao ya kijamii
- Wapo karibu sana na vijana na wanaelewa vizuri mahitaji ya vijana
- Wapo tayari muda wowote kukutana na kushauriana na vijana
Mapendekezo ya Marekebisho ya Muundo na Kanuni za Uendeshaji wa Kundi
- Mapendekezo ya Kuwepo kwa Kamati Mbalimbali
Zifuatazo ni Kamati ndogo zinazopendekezwa kufanya kazi na Viongozi wakuu wa kundi ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi;
i) Kamati Tendaji
Kamati Tendaji itaundwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu na Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Msemaji Mkuu, Wenyeviti wa Kamati Mbalimbali na Wanachama Waanzilishi wa Kundi.
Majukumu ya Kamati Tendaji ni
- Kusimamia mambo yote ya kundi pamoja na ushauri kwa kamati zote
- Kupokea taarifa mbalimbali za kamati na kuzitolea
- Kuandaa kalenda ya taratibu mbalimbali za chama
- Kuwa mwakilishi wa kundi sehemu yeyote kundi linapohitajika
- Kupokea na kutoa ushauri panapotokea kukinzana kwa wanachama au kamati ndogo ndogo
- Kuwa ni wasemaji wakuu wa
- Kuteua viongozi waandamizi wa kundi (Katibu, Katibu Msaidizi, Mwekahazina, Msemaji Mkuu wa Kundi, Viongozi na wajumbe wa Kamati Mbalimbali) kwa kuzingatia sifa zinazohitajika kwa ngazi husika
ii) Kamati ya Kuratibu Shughuli za Mitandao
Kazi ya kamati hii ni kuratibu shughuli zote zinazofanywa na kundi ikiwa ni pamoja na;
- Kuwa waendesha na wasimamizi wa shughuli za mitandao (Admins)
- Kuratibu zoezi la kuunganisha wanachama wapya kwenye mitandao
- Kuposti matukio na shughuli zote za utume kwenye mitandao
- Kufuatilia kila wakati kadiri iwezekanavyo matukio yanayoendelea kwenye majukwaa yote ya kundi mitandaoni na kuchukua hatua stahiki mara moja kunapotokea jambo linalokwenda kinyume na maadili ya kundi
Wafuatao wanapendekezwa kuunda kamati hii
- Majegero Selcious……….. Mwenyekiti
- Pauline Mlekani…………. Katibu
- Julian Mosha…………….. Mjumbe
- David Kiwasila………….. Mjumbe
- Nicholaus Mtakingilwa …Mjumbe
- Gordhard………………….. Mjumbe
- George Nkana……………. Mjumbe
- Albert Byengello………. Mjumbe
Kamati hii itasimamiwa na Makamu Mwenyekiti