LATEST ARTICLES

Jimbo kuu la Songea Lafanya Jubilei ya miaka 125 ya Uinjilisti

0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 01, 2023 amewasili katika Parokia ya Peramiho, jimbo kuu la Songea ambapo atashiriki katika Jubilei ya miaka 125 ya Uinjilisti katika Jimbo hilo.

Vatcan: Makardinali wapya 21 wasimikwa wakiwemo 3 kutoka Afrika

0

Viongozi wa Kikatoliki cheo cha Makardinali 21 wamesimikwa na Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis. Makardinali wapya hao wamesimikwa rasmi katika mkutano wa kawaida wa Baraza la Makardinali unaofanyika Jumamosi Septemba 30 mjini Vatican. Mnamo tarehe 9 Julai 2023 Baba Mtakatifu Francis aliwateua Makardinali wapya 21 kati yao Makardinali watatu wakiwa ni kutoka bara la Afrika ambao ni Askofu mkuu...

Papa Francis asisitiza kwamba serikali za Ulaya lazima zifanye zaidi kuwahudumia wahamiaji

0

Akifunga mkutano wa maaskofu na vijana kutoka eneo kuzunguka bahari ya Mediterania katika mji wa bandari wa Ufaransa wa Marseille, aliongeza kuwa uhamiaji ni hali halisi ya nyakati zetu Papa Francis siku ya Jumamosi alisisitiza ujumbe wake kwamba serikali za Ulaya lazima zifanye zaidi kuwahudumia wahamiaji wanaovuka bahari ya Mediterania, akisema wale wanaohatarisha maisha yao baharini hawavamii, bali wanataka kukaribishwa. Akifunga...

Papa Francis awataka Wakatoliki China kuwa wakristo wema

0

  Francis alitoa maoni hayo ambayo hayakuwa yameandikwa katika hotuba yake mwishoni mwa Misa katika mji mkuu wa Mongolia, akiwaita maaskofu wakuu wa zamani na wa sasa wa Hong Kong, Papa Francis alituma salamu kwa China siku ya Jumapili, akiwaita raia wake watu wa heshima na kuwataka Wakatoliki nchini China kuwa wakristo wema na raia wema katika ombi lake la hivi...

Papa Francis aelezea kusikitishwa na idadi kubwa ya wahamiaji wanaofia kwenye bahari ya Mediterranean

0

  Mkuu wa kanisa katoliki Papa Francis amesema Jumapili kwamba idadi ya wahamiaji wanaofia kwenye bahari ya Mediterranean ni ”jeraha la wazi”, kwa ubinadamu baada ya wiki nzima iliyogubikwa na mfululizo wa ajali za boti. Katika ibada ya kila wiki ya Angelus, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 86 aliwaombea watu 41 walioripotiwa kupotea Jumatano na wenzao wanne walionusurika na kupelekwa...

Papa Francis akutana na waathirika wa unyanyasaji wa kingono katika mkutano wa vijana katoliki duniani

0

Papa Francis Jumatano alisema kanisa katoliki linahitaji “kujitakasa kwa unyenyekevu na kwa muda mrefu” ili kukabiliana na “kilio cha uchungu” cha waathirika wa unyanyasaji wa kingono waliotendewa na makasisi. Alikutana na waathirika hao kwa faragha jana Jumatano katika siku ya kwanza ya ziara yake nchini Ureno. Francis alikuwa akizungumza mjini Lisbon mwanzoni mwa ziara ya siku tano nchini humo ambayo anatumai...

Papa asema ahofia matukio ya moto nchini Ugiriki

0

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis leo ameeleza wasiwasi juu ya matukio ya moto inayoikumba Ugiriki na mataifa mengine duniani. Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis aidha amewahimiza watu kuongeza juhudi za kuitunza dunia. Kupitia ujumbe uliotumwa na Vatican, Papa Francis ameonyesha kusikitishwa na tishio kwa maisha ya binadamu na uharibifu unaosababishwa na moto unaoenea kwa kasi nchini...

Papa Francis arejelea majukumu yake baada ya kufanyiwa upasuaji

0

  Siku mbili baada ya kuondoka hospitalini, kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki, Papa Francis alianza tena desturi yake adhimu ya Jumapili, ya kusalimia umma katika uwanja wa St. Peters. Alianzia kwa kuonekana dirishani akisema kwamba ukaribu wa kibinadamu na wa kiroho aliohisi alipokuwa hospitalini, akifanyiwa upasuaji wa tumbo ulimpa "faraja kubwa." Maelfu ya mahujaji na watalii katika uwanja huo, walishangilia kwa kupiga...

Papa Francis, 86, kufanyiwa upasuaji wa tumbo

0

Papa Francis atafanyiwa upasuaji wa tumbo lake Jumatano alasiri katika hospitali ya Gemelli ya Roma. Anatarajiwa kukaa hospitalini kwa "siku kadhaa" ili kupata nafuu kutokana na upasuaji wa mishipa iliyovimba au ngiri, Vatican imesema. Tatizo hilo "linasababisha maumivu makali sana ya mara kwa mara," msemaji wa Vatican Matteo Bruni aliongeza. Mzee huyo mwenye umri wa miaka 86 amekabiliwa na msururu wa matatizo...

Zelensky yuko Roma kukutana na Papa Francis

0

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky yuko Roma ambapo anakutana na viongozi wa kisiasa na amekutana na Papa Francis. "Ziara muhimu kwa ushindi unaokaribia wa Ukraine!" Zelensky aliandika kwenye mtandao wake wa twitter alipotua katika mji mkuu wa Italia. Atakutana pia na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, Rais Sergio Mattarella na kuelekea hadi Vatican baadaye Jumamosi. Kumekuwa na usalama mkubwa, na zaidi...