WAMISIONARI WAKATOLIKI MTANDAONI (ZAMANI VIJANA WAKATOLIKI TANZANIA) RIPOTI MAALUM YA SHUGHULI ZA UTUME NA UINJILISHAJI TOKA KUNDI LILIPOANZISHWA 2010 HADI SASA 2022
Imeandaliwa na Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni Septemba 2022
Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni ni kikundi cha Wakatoliki kilichonazishwa Jimboni Arusha mwaka 2010 na baadae kuenea katika majimbo mablimbali nchini Tanzania. Wamisionari wameunganishwa kupitia mitandao ya kijamii.
Hadi sasa tuna utume umesambaa katika majimbo kadhaa ikiwemo Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Shinyanga, Kahama, Iringa, Tanga, Dodoma na Mpanda ambayo yana uongozi kamili. Kuna majimbo mengine yana utume lakini mwamko bado haujawa mzuri hivyo tunaendelea kuhamasishana.
Utume huu umejikita zaidi katika kufanya Matendo ya Kiinjili ya Upendo na katika majimbo ambayo tunafanya utume, tunasimamiwa na mapadre kiroho. Pia tunaye Padre mlezi wa Taifa Padre Timoth Nyasulu Maganga ambaye tuko nae bega kwa bega katika katika shughuli za Utume huu.
Mwaka 2017, utume huu ulitambuliwa rasmi na Mwadhama Kardinali Pengo wakati huo akiwa ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. Hata alipostaafu, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Baba Askofu Mkuu Yuda Thaddaeus Ruwa’ichi ameendelea kuwa nasi bega kwa bega na utume huu.
Kikundi kina utaratibu wa kufanya Matendo ya Upendo mara mbili kila mwaka. Matoleo ya kwanza yanafanyika kipindi cha Kwaresma na Mateloo ya Pili kipindi cha Majilio.
Yafuatayo ni Matendo Ya Upendo ambayo yamefanyika tangu kuanzishwa kwa Utume huu
⦁ Kituo cha Watoto Yatima cha Mburahati Charity Centre, Jimbo Kuu Katoliki, Dar es Salaam (Januari 2012)
Moja ya picha muhimu sana katika historia ya Kundi letu. Vijana hawa wawakilishi ndio walianzisha safari ndefu ambayo mpaka sasa imechukua miaka zaidi ya 11 ya kutembelea na kusaidia wahitaji na kufanya Utume katika kanisa
⦁ Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Dar es Salaam (Mei 2012)
Kituo cha Kulelea watoto Yatima cha Joshua Christian School, Arusha (Januari 2013)
Kituo cha Kulelea Watoto walemavu na wenye Mtindio wa Ubongo cha Amani, Jimbo Katoliki la Morogoro (Aprili 2013)
Kituo cha watoto yatima cha Nyumba ya Furaha (Cassa dell Gioia), Jimbo Katoliki la Tanga (June 2014)
Watoto Wagonjwa wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam (December 2014)
Kituo cha Watoto wenye ulemavu wa ngozi cha Buhangija, Jimboni Shinyanga, April 26-28, 2018
Mwanzoni mwa mwaka 2017, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu wa Jimbo
Kuu la Dar es Salaam alifanya maamuzi yaliyotushangaza ya kuutambua utume wetu na kutuunganisha rasmi kufanya kazi kwenye Jimbo la Dar es Salaam pamoja na Shirika la Kipapa
la Utoto Mtakatifu. Tokea wakati huo tumekuwa tukishirikiana na Walezi pamoja na Utume wa
Utoto Mtakatifu kuinjilisha.
Tulianza kwa kushiriki Kongamano la Utoto Mtakatifu Kanda ya Mashariki na Pwani
lililofanyika Zanzibar mwezi June 2017 pamoja na kisha tukashirikiana nao kuchangia Uchimbaji
wa Kisima cha Maji Safi katika Mahabusu ya Watoto ya Upanga jijini Dar es Salaam.
Tumeendelea kufanya kazi na Utoto Mtakatifu katika matukio mengine mengi ya uinjilishaji.
Lengo letu la baadae ni kuhakikisha mtindo huu wa kufanya kazi unaenea katika majimbo
mengine
Kongamano La Utoto Mtakatifu Kanda ya Mashariki na Pwani – Zanzibar (2017)
Wawakilishi kwenye Kongamano la Utoto Mtakatifu Kanda ya Mashariki na Pwani
lililofanyika Jimbo Katoliki la Zanzibar June 10, 2017
Aidha tunajivunia kuwa k ati ya wadau waliokuwa mstari wa mbele kuhakikisha
filamu iitwayo SISTER MARY, ambayo kwa macho yetu ilikuwa ikidhalilisha
Ukatoliki iliyotarajiwa kusambazwa mwaka 2013 haitoki. Harakati zetu ziliwezesha
filamu hiyo kuzuiwa kusambazwa.Pia, tulijaribu kuhamasisha kukomeshwa kwa mauaji na dhuluma mbalimbali dhidi ya makasisi na
viongozi wengine wa kanisa, mambo yaliyoshika kasi hapo mwaka 2015.
⦁ Gereza la Wafungwa la Mbozi - Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya (May 2019)
. Katika Kituo cha Kevina Hope Centre – Same (Desemba 2019
⦁ Kituo Cha Hija – Karema (Mpanda) June 2022
Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka (Matendo ya Upendo katika kipindi cha Kwaresma) kama ilivyo utaratibu, Mungu ametuwezesha kumjengea mama Bikira Maria Grotto hapa Karema kwa ushirikiano wa karibu na Askofu wa Jimbo na waumini wa Karema.
Kuelekea kwenye Grotto hili, kumejengwa vituo vya njia ya msalaba pia.
Zifuatazo ni picha za matukio tofauti katika kukabidhi Grotto hili na Baraka kutoka kwa Askofu wa Jimbo la Mpanda Eusebius Nzigilwa.