Papa Francis, Jumamosi alifanya maboresho ya sheria ya kanisa ya 2019 inayolenga kuwawajibisha wakuu wa makanisa kwa kuficha kesi za unyanyasaji wa ngono.

Amefanya iwe pana zaidi ili kuwawajibisha viongozi wa kanisa Katoliki na kusisitiza kwamba watu wazima walio katika mazingira magumu wanaweza pia kuwa waathirika wa manyanyaso pale wanapo shindwa kuridhia jambo fulani.

Papa Francis alithibitisha tena na kufanya vifungu vya muda vya sheria ya 2019 vilivyopitishwa wakati wa sakata la viongozi wa Vatican na uongozi wa kanisa Katoliki.

Sheria hiyo ilipongezwa wakati huo kwa kuweka utaratibu sahihi wa kuwachunguza maaskofu na wakuu wa dini, lakini utekelezaji wake umekuwa usio na uwiano, na Vatican imekosolewa na waathirika wa unyanyasaji kwa kuendelea kukosekana kwa uwazi kuhusu kesi hizo.