Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan amekutana mjini Dodoma na Balozi wa Vatican nchini Tanzania,Askofu Mkuu Accattino wakati wa kuwasilisha hati ya utambulisho wake Jumatatu tarehe 27 Februari 2023.
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Balozi wa Vatican, Askofu mkuu Angelo Accattino aliteuliwa mnamo tarehe 2 Januari 2023 na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Tanzania. Kabla ya uteuzi huo, Askofu Mkuu Accattino alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Bolivia. Kwa njia hiyo Jumatatu tarehe 27 Februari 2023, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi Samia Suluhu Hassan, amekutana na Wanadiplomasia huko Ikulu Chamwino, Dodoma na miongoni mwao amekutana kwa mara ya kwanza katika kuwakilisha Hati yake ya Utambulisho na Askofu Mkuu Accattino.
Rais wa Jamhuri ya Tanzania amepokea hati za
Rais wa Jamhuri ya Tanzania amepokea hati za
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa wa Mawasiliano ya Ikulu Tanzania, inabainisha kuwa: “katika mazungumzo yao na Bi Suluhu Hassan, wamejikita kutazama juu ya ushirikiano zaidi katika masuala ya Afya, Elimu, Mazingira na Amani.” Hata hivyo ikumbukwe kwamba Askofu mkuu Angelo Accattino alizaliwa tarehe 31 Julai 1966, Jimboni Casale Monferrato, nchini Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre mnamo tarehe 25 Juni 1994 alipewa Daraja Takatifu ya Upadre. Askofu mkuu Angelo Accattino alianza utume wake katika masuala ya kidiplomasia ya Vatican, rasmi mnamo tarehe 1 Julai 1999. Na Baba Mtakatifu Francisko mnamo tarehe 12 Septemba 2017 alimteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Bolivia na kumpandisha hadhi kuwa ni Askofu mkuu na wakati huo huo kuwekwa wakfu kama Askofu mkuu mnamo tarehe 25 Novemba 2017.
Rais pia alikutana na Balozi wa Ufilipino pamoja na Romania
Kwa hiyo tukirudi tena katika mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mabalozi wengine ni pamoja na Balozi wa Ufilipino, Bi Marie Charlotte G. Tang nchini Tanzania ambaye mara baada ya kupokea hati yake ya utambulisho, walizungumza na Rais masuala ya kilimo na uvuvi, sekta ambazo nchi hiyo imepiga hatua kubwa. Kadhalika Rais Samia alipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi Gragos- Viorel–Radu Tigau wa Romania nchini Tanzania. Katika mazungumza yao, kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, imebanisha kuwa yalijikita “katika sekta ya Elimu na Teknolojia”. Kuhusiana na hilo kwa hakika nchini Romania inaongeza ushindani mzuri duniani katika nyanya za teknolojia ya habari (TEHAMA).