Uharibifu na kufuru umetokea katika Kanisa Kuu Katoliki la Geita,nchini Tanzania ambapo Askofu Kassala,wa Kanisa hilo alitangaza Dominika tarehe 26 Februari 2023.Wahusika wa tukio hilo baya wako mikononi mwa vyombo vya umma na upelelezi unaendelea.Askofu na waamini wanasikitika kuhusu tendo hilo.
Na Angella Rwezaula;- Vatican.
Usiku wa manane kuamkia Dominika ya Kwanza ya Kwaresima, tarehe 26 Februari 2023, Kanisa Kuu la Geita nchini Tanzania, lilipata uharibifu mkubwa. Taarifa hizo zilitolewa na Askofu Flavian Matindi Kassala wa Jimbo hilo kwa kutuma ujumbe wake kuhusiana na tendo hilo baya ambalo lilioneshwa pia uharibifu huo kwa njia ya video fupi na picha katika Kanisa Kuu na sehemu zake.
Kwa mujibu wa Askofu Kassala alifafanua jinsi ya uvunjaji wa lango Kuu la Kanisa lilivyokuwa. Na wakati huo huo mhusika aliyefanya hivyo alisema alivyokamatwa na ameshikiliwa na vyombo vya umma kwa ajili ya upelelezi zaidi.
Kanisa Katoliki Jimbo Kuu ka Geita limepata mkasa wa kuharibiwa matakatifu
Kanisa Katoliki Jimbo Kuu ka Geita limepata mkasa wa kuharibiwa matakatifu
Pamoja na hayo kupitia vyombo vya habari mahalia. (Mwanchi digitali) imefanya mahojiano na Askofu Kasala na kuelezea hali halisi ilivyo na masikitiko ya uharibifu wa vyombo muhimu na vitakatifu katika Kanisa hilo. Vile vile hata maoni ya baadhi ya waamini wa Kanisa Kuu hilo na masikitiko yao, Dominika hiyo hiyo.
Je huyo mtu ni nani na ana makusudi gani?
Tunabaki na mshangao na maswali ya kujiuliza: Je huyo ni nani? Ametumwa na nani? au alikuwa na nani wakati wa tukio hilo bovu? Hakuna kinachoumiza na kushangaza sana kuhusu matukio kama haya mabaya ya kugusa kiungo cha Kikanisa na hasa kuhusiana na mambo matakatifu hasa kwa upande wa wakatoliki!
Tabernakulo ikiwa imevunjwa vunjwa ndani ya Kanisa Kuu Geita nchini Tanzania