Kuanzia Januari 16, 2023 Nauli ya Mabasi ya Mwendokasi itakuwa Tsh. 750 kutoka 650, njia ya mlisho (Feeder Route) ni Tsh. 500, njia ya mlisho na njia kuu (Feeder & Truck Route) Tsh. 900 njia ya Kimara – Kibaha ni Tsh. 700 badala ya pendekezo la DART la Tsh. 1,200

Teksi Mtandao za abiria 4 Tsh. 3,000 – 4,000, Magari ya abiria 6 itakuwa Tsh. 4,000 – 5,000 ndani ya Kilomita 1, na safari ikizidi itaongezeka kwa Tsh. 800 hadi 1200 kwa kilomita 1. Ikiwa kutakuwa na vikwazo kama foleni nauli itaongezeka kwa Tsh. 80 hadi Tsh. 150 kwa kila dakika

Pikipiki za abiria 2 nauli itakuwa Tsh. 1,000 – 1,500, Pipipiki za abiria wasiozidi 3 itakuwa Tsh. 2000 – 2500 ndani ya Kilomita 1, na safari ikizidi itaongezeka kwa Tsh. 300 – 600 kwa kila kilomita moja na kama kutakuwa na vikwazo kama foleni nauli itaongezeka kati ya Tsh. 50 hadi 90 kwa kila dakika.