Mazishi ya Benedict XVI yatafanyika Alhamisi Januari 5, 2023 na yataongozwa na Papa Francis, Vatican imesema.

Kiongozi wa Ujerumani atoa salamu za risala kwa mjerumani mwenzake

Benedict wa 16 ameelezewa kuwa mtu mwenye mzuri na Mjerumani mwenzake, Kansela Olaf Scholz.

Scholz alituma ujumbe wa Twitter akisema Papa huyo wa zamani alikuwa “kwa wengi, sio tu katika nchi hii, kiongozi maalum wa kanisa” Anasema mawazo yake yako kwa papa wa sasa, Francis.