Moyo Safi Wa Bikira Maria Kimbilio Na Faraja Kwa Wanaoteseka!

 Moyo Safi Wa Bikira Maria Kimbilio Na Faraja Kwa Wanaoteseka!

Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Sherehe ya Bikira Maria Kupashwa habari kuwa atakuwa ni Mama wa Mungu ameadhimisha Ibada ya toba na maondoleo ya dhambi sanjari na kuiweka Urussi na Ukraine wakfu kwa maombezi ya Moyo Safi wa Bikira Maria. Hili ni tukio ambalo limeadhimishwa sehemu mbalimbali za dunia kama kielelezo cha ushirika wa Kanisa la Kristo.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Ee Bikira Maria, Mama wa Mungu na Mama yetu, sisi, katika saa hii ya dhiki, tunakukimbilia. Wewe ni Mama, unatupenda na unatujua: hakuna kitu kilichofichwa kwako kutoka nyoyoni mwetu. Mama wa huruma, mara nyingi tumeonja huruma yako ya upendo, uwepo wako unaoturejeshea amani, ili utuongoze daima kwa Yesu, Mfalme wa amani.

 

Lakini tumepoteza njia ya amani. Tumesahau somo la majanga ya karne iliyopita, dhabihu ya mamilioni ya watu walioanguka katika Vita Kuu ya Dunia. Tumepuuza ahadi zilizotolewa kama Jumuiya ya Kimataifa na tunasaliti ndoto za amani za watu na matumaini ya vijana.

 

Tumeugua kwa tabia ya uchoyo, tumejifungia kwa maslahi ya utaifa, tumejiruhusu kulemazwa na hali ya kutojali na kudhohofishwa na ubinafsi. Tulipendelea kumpuuza Mwenyezi Mungu, kuishi na uwongo wetu, kuchochea uchokozi, kukandamiza uhai na kulimbikiza silaha, tukisahau kwamba sisi ni walinzi wa jirani yetu na mazingira nyumba ya wote.

 

Tumeirarua bustani ya dunia vipande vipande kwa vita, tumeujeruhi moyo wa Baba yetu kwa dhambi, ambaye anataka tuwe ndugu wamoja. Tumekuwa watu wasiojali kila mtu na kila kitu isipokuwa sisi wenyewe. Na kwa aibu tunasema: utusamehe, Bwana!

Katika taabu ya dhambi, katika juhudi na udhaifu wetu, katika fumbo la uovu na vita, wewe, Mama Mtakatifu, unatukumbusha kwamba Mwenyezi Mungu hatutupi, bali anaendelea kututazama kwa upendo, akitamani kutusamehe na kuamka tena. Yeye ndiye aliyetupatia wewe na ameweka katika Moyo wako Safi kimbilio kwa Kanisa na kwa wanadamu. Kwa wema wa kimungu uko pamoja nasi na hata katika mikunjo finyu ya historia unatuongoza kwa upole.

Basi na tunakimbilia kwako, tuubishe mlango wa Moyo wako Safi, watoto wako wapendwa ambao hawachoki kutembelea na kuwaalika kwenye wongofu. Kanisa katika saa hii ya giza, njoo utusaidie na kutufariji.

 

Rudia kwa kila mmoja wetu: “Je, mimi si niko hapa, Mama yako ni nani?” Wewe unajua jinsi ya kufungua kinzani ya mioyo na mafundo ya nyakati zetu.

Tunaweka imani yetu kwako. Tuna hakika kwamba wewe, haswa wakati wa majaribio, hutadharau maombi yetu na uje hima kutusaidia. Hivi ndivyo mlivyofanya kule Kana ya Galilaya, mlipoharakisha saa ya Yesu kuingilia kati na kufanya ishara yake ya kwanza ulimwenguni.

 

Sikukuu ilipogeuka kuwa huzuni ulimwambia: “Hawana divai” (Yn 2: 3). Rudia tena kwa Mwenyezi Mungu, Ee Mama, kwa sababu leo tumetindikiwa na divai ya matumaini, furaha imetoweka, na udugu umesambaratika. Tumepoteza ubinadamu na tumepoteza amani. Tumekuwa na uwezo wa vurugu na uharibifu wote. Tunahitaji uingiliaji wako wa kina, Mama fanya haraka.

Leave a Reply

Your email address will not be published.