Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumamosi tarehe 26 Machi 2022, Baba Mtakatifu Francisko amekutana katika Jumba la Kitume la Rais wa Jamhuri ya Burundi Bwana Évariste Ndayishimiye, ambaye mara baada ya mkutano huo amekutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Uhusiano na Ushirikiano na Nchi.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari Vatican, wakati wa mazungumzo na Katibu wa Vatican wamepongezana kuwa na mahusiano mema kati ya Vatican na Burundi, na mchango wa Kanisa katoliki unaotolewa katika maisha ya Nchi na kwenye sekta mbali mbali za kijamii. Katika mazungumzo hayo pia wamegusia kuhusu hali za sera za kisasa na kijamii katika Nchi na wamekabiliana na mantiki zenye tabia za kikanda.

Na kwa upande wa zawadi za Rais wa Burundi kwa Papa vilikuwa ni vyombo vya muziki wa asili nchini Burundi na Uthibitisho wa mchango wa ujenzi wa kanisa nchini Burundi.