Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji limekusanya ushuhuda wa Askofu Mkuu Visvaldas Kulbokas,Balozi wa Vatican,ambaye amebainisha kuishi katika vita kwa hakika ni kitu kigumu lakini mshikamano ni mkubwa kwa wakatoliki,waorthodox na waislamu ambao wanatafuta kufikia watu kwa ugumu,kugawa chakula,na kusaidia kuondoka kwa yule ambaye yuko katika matatizo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Askofu Mkuu Visvaldas Kulbokas, Balozi wa Vatican huko Ukraine, wakati wa mahojiano yaliyokusanywa na Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji amesema “Mgogoro wa kibinadamu ni mkubwa sana na ninabeba wasiwasi huu moyoni mwangu, na si mara zote inawezekana kusaidia. Wakati mwingine hata mashirika kama Caritas au Msalaba Mwekundu hawawezi kufanya kitu”. Askofu kwa hakika amejaribu kutoa nuru kwa kile ambacho kimetokea tangu siku za kwanza baada ya kuzuka kwa mzozo huo na pia juu ya shida zinazowakabili, na kuonesha kwa dhati mchango wa mashirika mengi, sio tu ya Kikatoliki, pia ya Kiorthodox na Waislamu, ambayo yanajikita binafasi kuwafikia watu wengi katika shida na kugawa chakula huku wakitafuta kwa ugumu sana kuwahamisha wale ambao wako katika hali ngumu zaidi, labda kutoka mahali ambapo hawana umeme na joto. Kutokana na hivyo Balozi wa Vatican aamethibitisha juu ya mshikamano wa nguvu uliopo!

Askofu Mkuu Kulbokas ameeleza kwamba Yeye anatumia muda mwingi kukaa kwenye simu ili kujibu katika kuandaa misaada na kushughulikia maombi ya dharura kwa watu. “Kuna wasiwasi mwingi, meongeza kuwa watu wanaonesha ujasiri kwamba

“Tunahisi kwamba lazima tukabiliane na janga hili pamoja, tusaidiane na tuombeane sana. Walakini, tunaishi katika hali ya halisi ngumu ambayo utafikiri kama kwenye sinema, kwa sababu hii inajieleza yenyewe pia kwa waamini wengi kwamba silaha zao kuu ni unyenyekevu, kujiachia kabisa kwa Mungu, mshikamano na ‘upendo”.

 

Katika vita hii ambayo amesisitiza Balozi, kuna kitu moja, kwamba sisi sote tunaweza kujibu kwa pamoja kwa kufunga, kwa maombi, kwa unyenyekevu mwingi na upendo. Nyakati hizi za vita zinatusukuma kama nabii asemavyo Isaya kutazama kwa Mungu wetu kwa macho mapya, kwa macho ya uaminifu, unyenyekevu na uongofu. Ukaribu wa Papa, sio tu kwa maneno bali kwa vitendo, pia unaonekana sana, kwani ametuma makadinali wawili katika eneo hilo. Baadaye kuna ukaribu wa Misaada kwa Kanisa hitaji msaada ambalo limetenga kiasi cha euro milioni 1.3 kwa majimbo yenye uhitaji hasa kusaidia kazi za mapadre na watawa. Askofu Mkuu Kulbokas ana hakika kwamba katika siku zijazo kazi muhimu itabidi ifanywe “katika ngazi ya kimuundo na ya shirika kwa sababu kuna mamia ya shule, hospitali, nyumba zilizoharibiwa. Mahitaji yatakuwa makubwa sana. Itachukua muda mrefu kurudi kwa hali kaka kawaida”.