Papa Francisko katika katekesi yake Jumatano 7 Aprili amejikita kufafanua kuhusu sala na muungano wa watakatifu.Tunaposali hatuko peke yetu bali tunalo kundi la watakatifu ambalo linatutangulia kuomba kwa Yesu Kristo.Mtakatifu ambaye hakurejeshi kwa Yesu Kristo sio mtakatifu,na si Mkristo.Utakatifu ni njia ya maisha,ya kukutana na Yesu iwe kwa muda mrefu na mfupi

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Katika katekesi yake Papa Jumatano tarehe 7 Aprili 2021 amependa kujikita kutazama juu ya uhusiano kati ya sala na Muungano wa watakatifu.  Na ni kwa sababu, anasema tunapokuwa tunasali, hatufanyi kamwe peke yetu, hata kama hatufikirii hivyo, lakini tumo ndani ya mto wa nguvu wa maombi ambayo yanatanguliwa na kufuatia sisi. Mto mzuri. Katika sala tuazokutana nazo katika Biblia, na mara nyingi zinasikika katika liturujia, kuna njia ya historia za kizamani, miujiza ya kukombolewa, kupelekwa utumwani na huzuni wa uhamishoni, kumbu kumbu na  majuto, sifa mbele ya mshangao wa uumbaji… Na hivyo sauti hii zikarithishwa kizazi hadi kizazi, katika msukano kati ya uzoefu binafsi na ule wa watu na jumuiya ambayo walikuwamo. Hakuna ambaye angeweza kutengena na historia binafsi, historia ya watu wake na daima katika mazoea ambaye tunapokea urithi na hata katika sala.

Katika sala ya kusifu, kama ile njema ambayo inatoka ndani ya moyo wa wadogo, na wenyenyekevu, inajikita katika jambo moja la wimbo wa Sifa ambayo Maria aliinua kwa Mungu mbele ya ndugu yake Elizabeth; au maneno ya mzee Simeoni ambaye mara baada ya kumshika mtoto Yesu mikononi mwake  alisema “ Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema” (Lk 2,29). Maombi ambayo ni mazuri ni yale yanayoendelea kuwa au bila ujumbe wa njia ya kijamii katika njia za hospitali, katika wakati mzuri wa sala kama hata ule wa mateso katika ukimya… Uchungu wa kila mmoja ni uchungu wa wote, na furaha ya mmoja inakuwa katika roho za wengine. Uchungu na fautah , historia yote na ambayo inatufanya kuwa historia ya maisha binafsi ni kuiishi tena na maneno yake lakini katika uzoefu wenyewe.

Maombi yanazaliwa daima tunapofunga mikono na kufungulia moyo kwa Mungu, tunajikita katika usindikizwaji wa watakatifu wasiojulikana na watakatifu wanaoujulisha ambao wanasali nasi, na kwa ajili yetu wanaomba kama kaka na dada wakiwa katika mchakato wa safari ya kibinadamu.  Katika Kanisa hakuna maombolezo ambayo yanabaki yametengwa, hakuna chozi linaloanguka bure, kwa sababu kila kitu kinapumua na kushiriki neema ya pamoja. Si kwa bahati mbaya katika makanisa ya kizamani, maziko yalikuwa yakifanyika katika bustani karibu na nyumba takatifu, kama kuonesha  kuwa kila Ekaristi wanayoshiriki kwa namna moja, wanashiriki hata na kikundi cha wale wote waliotangulia. Wapo wazazi wetu, babu na bibi zetu, wapo wasimamizi wa ubatizo, wapo makatekisti na walimu… Imani hiyo iliyokabidhiwa, iliyopitishwa na kurithishwa, ambayo tumepokea na kwamba kwa imani pia imepitishwa  kuomba na sala.

Watakatifu bado wapo hapa na hawako  mbali nasi; picha zao zilizomo katika Makanisa zinaomba kama lile wingu kubwa linalotuzunguka  la mashahidi namna hii ( Eb 12,1). Hao ni mashuhuda ambao hatuwaabudu, lakini tunawaheshimu na kwa namna nyingi tofauti wanatuelekeza kwa Yesu Kristo Bwana mmoja na Mwombezi kati ya Mungu na mtu. Mtakatfui hasiyeeleza kwa  Yesu Kristo sio Mtakatifu na si Mkristo. Mtakatifu anakufanya ukumbuke Yesu Kristo kwa sababu yeye alipitia nja ile ya kuishi kama Mkristo. Watakatifu wanatukumbusha kuwa hata maisha yetu pamoja na udhaifu na wenye dhambi, tunaweza kuchanua utakatifu.  Hakika, wakati wa mwisho pia. Kwa bahati katika Injili tunasoma kwamba mtakatifu wa kwanza aliyetangazwa alikuwa mwizi na hakutangazwa na Papa, bali na Yesu mwenyewe. Utakatifu ni njia ya maisha, ya kukutana na Yesu, iwe kwa muda mrefu na mfupi.  Lakini daima ni ushuhuda, mtakatifu ni shuhuda, wa mwanamume, mwanamke aliyekutana na Yesu na aliyemfuata Yesu. Haijawahi kuchewelea kuongokea Bwana, ambaye ni mwema, Bwana amejaa huruma ni mwingi wa fadhili ( Zab 102,8)

Katika katekisimu inaeleza kuwa watakatifu “wanamtafakari Mungu , wanamsifu na hawaachi kutunza wale ambao waliwaacha duniani (…) Maombi yao yako juu zaidi katika huduma ambayo inakupeleka ishara ya Mungu. Tunaweza na lazima kuwaomba maombezi yao kwa ajili yetu na kwa ajili ya ulimwengu mzima” (KKK2683). Katika Kristo kuna siri moja ya mshikamano kati ya wale waliotangulia katika maisha mengine na sisi wanahija katika Dunia hii. Kwa ndugu zetu marehemu, kutoka Mbinguni wanaendelea kututunza. Wao wanasali kwa ajili yetu na sisi tunasali kwa ajili yao. Husiano huu wa sala kati yetu na watakatifu yaani kati yetu na watu ambao umefikia kuwa huhusiano wa sala  tunazofanyia uzoefu tayari hapa katika maisha ya dunia. Tusali kwa ajili ya wengine, tuombe na kutoa sala…. Namna ya kwanza ya kusali kwa ajili ya mtu ni kuzungumza na Mungu juu yake. Ikiwa tunafanya hivyo kila wakati, kila siku, moyo wetu hauwezi kufungwa, unabaki umefunguka kwa ndugu. Kusali kwa ajili ya wengine ndiyo namna ya kuwapenda na kutusukuma katika ukaribu wa dhati. “Hata wakati wa mizozo, njia moja ya kumaliza mzozo, kuulainisha, ni kumuombea mtu ambaye ninapingana naye. Na kitu hubadilika kwa sala. Jambo la kwanza linalobadilika ni moyo wangu, ni mtazamo wangu. Bwana huubadilisha ili kuruhusu (kufanikisha) kukutana, mkutano mpya na kuzuia mzozo kuwa vita visivyo na mwisho”.

Mtindo wa kwanza wa kukabiliana katika wakati mgumu ni ule wa kuomba ndugu, hasa watakatifu, ambao wanasali kwa ajili yetu. Jina ambalo tulipewa wakati wa ubatizo siyo lebo au pambo! Ni kwa kawaida ni jina la Bikira, la mtakatifu wa kike au kiume, ambao hawasubiri kingine zaidi ya kutaka kutusaidia ,ili kupata kutoka kwa Mungu neema ambayo tunahitaji. Ikiwa katika misha yetu ya majaribu hatujaweza kupata nafuu na ikiwa bado tuna uwezo wa kuvumilia;  ikiwa kwa bahati tunakwenda mbele kwa imani na kama ingekuwa kila kitu hicho na zaidi tunastahili tunapaswa kuwaomba watakatifu wengine, baadhi wako mbinguni, na wengine wako pamoja nasi hapa duniani, wakitulinda na kutusindikiza. Kwa sababu sisi sote tunajua kuwa hapa duniani kuna watu watakatifu, wanaume na wanawake watakatifu wanaoishi katika utakatifu, hawajui, wala sisi hatujui lakini kuna watakatifu, watakatifu wa kila siku, watakatifu waliofichwa au kama Papa amesisitiza kuwa mara nyngi aansema  “watakatifu wa karibu”, wale ambao wanaishi nasi maishani, ambao hufanya kazi na sisi, na wanaishi maisha ya utakatifu. Kama alivyosema Mtakatifu Basilio katika shajara la kiroho kuwa  “Ahimidiwe Yesu Kristo, Mwokozi wa pekee wa ulimwengu, pamoja na maua haya makubwa ya watakatifu wote  ambao wamezunguka dunia na ambao wamefanya maisha yao kuwa sifa kwa Mungu. Ni makao yanayofaa zaidi, kwani wanajitoa kuishi na Mungu amewaita katika hekalu lake” amehitimisha.