Unahitaji kuwafanya wateja wako wawe na furaha. Unahitaji kuwafanya wawe wateja wanaokuja kwako kila mara na waweze kuleta marafiki zao.
Kama utakuwa na wateja wasio na furaha, wanaweza wakasambaza maneno ya siyo mazuri kuhusu biashara yako kwa watu wengine.
Sasa unafanya nini kuhakikisha wana furaha na biashara yako? Jitahidi kuwafanya wateja wako wapende wanachopata kutoka kwako. Jifunze kuhusu wateja wako; ili kufanya kupenda biashara yako, kwanza unahitaji kujua wanachotaka.
Anza kwa kutafuta wateja wako wanataka nini kwa kuchunguza nini kipo sokoni na nini hakipo. Wakati wa kuchunguza kuhusu soko, unatakiwa kutafuta kujua juu ya mahitaji, matakwa, maslahi na hitaji la wateja wako. Ukijua wanachotaka, utaweza kuwapa.
Mfano; kama umetafiti na kugundua sehemu f ’lani kuna uhaba wa viatu vya ngozi, ni na uhusiano binafsi na wateja, usiwe roboti.
Usitumie majibu ya kiautomatiki kwa wateja wako wa karibu. Hakuna mteja atakayefurahi kukutumia ujumbe kisha akajibiwa na ujumbe wa ki-automatiki uliosetiwa kwenye kompyuta. Tafuta njia za kuonesha tabia ya biashara yako na ujumuishe wateja ndani yake, hata ikiwa katika ujumbe unaowatumia.
Toa ofa na madili ya kuvutia. Watu wengi wanapenda madili kama vile punguzo la bei na ofa. Wateja wakiona wanapata thamani za pesa zao katika madili na ofa za bidhaa zako, watakuwa na uwezekano mkubwa wa kurudi.Unaweza kutoa punguzo na madili mengine wakati wa sherehe za msimu wa mwaka.
Au unaweza kutoa bidhaa za bure kwa wateja wazijaribu, au ile ya nunua moja upatemoja bure.
Uuzaji huo huhamasisha wateja kuendelea kurudi kwenye biashara yako. Wakati watu wanapenda madili na punguzo kwenye bidhaa zako, watapenda biashara yako zaidi.Hata kama ofa na madili yanaweza kukusababisha usipate faida kwa sasa,