Mara baada ya Katekesi yake Papa Francisko amekumbusha siku ya Kimataifa ya Mchezo kwa ajili ya Maendeleo na Amani ilioyofanyika tarehe 6 Aprili na kuongeza kuwatia moyo wanariadha wa Vatican ili kuendelea kueneza utamaduni wa udugu.

 

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jumatano tarehe 7 Aprili 2021, mara baada ya Katekesi yake na wakati wa salamu, Papa Francisko ametoa wito kuwa kuwa “Jana ilikuwa Siku ya Kimataifa ya Michezo wa Maendeleo na Amani, iliyotangazwa na Umoja wa Mataifa. Natumai kuwa inaweza kuzindua tena uzoefu wa mchezo kama hafla ya timu, ili kukuza mazungumzo ya mshikamano kati ya tamaduni tofauti na watu.

 

Akiendelea Papa Francisko katika muktadha huo amesema “Kwa mtazamo huu, ninapendelea kuwatia moyo Wanariadha wa Vatican ili kuendelea kujitoa katika jitihada ya kueneza utamaduni wa udugu katika mantiki ya michezo, kwa kuzingatia sana watu walio dhaifu kwa maana hiyo kuwa mashuhuda wa amani”.