Matashi mema kutoka pande zote za dunia yamefika kwa sababu ya miaka 8 ya upapa kwa kuishi na furaha ya Injili.Wanaandika maaskofu wa (CELAM), kwenye tukio la maadhimisho yake tangu achaguliwe kuwa Papa.

Kardinali De Donatis,makamu wake anamtakia mema kwamba amefanya wagundue,mafundisho na ushuhuda wake wa maisha,furaha tamu na yenye kufariji katika kuinjilisha.

 

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Miaka minane ya upapa kwa kuishi na furaha ya Injili ndivyo wanaandika maaskofu wa shirikisho la mabaraza ya Maaskofu wa Amerika Kusini (CELAM), kwenye tukio la maadhimisho ya Miaka minane tangu Papa Francisko achaguliwe tarehehe 13 Machi 2013- 13 Machi 2021, ambapo wanakumbusha kuwa kwa mara ya kwanza alionekana katika ubaraza mbele ya Kanisa Kuu la Mtaktifu Petro akijitambulisha kwa ulimwengu kama Mfuasi wa Petro. Hii ndiyo maana ya fursa ya kumtumia ujumbe wa matashi mema.

Kwa shukrani kutoka kwa maaskofu wa Celam, wanaelezea hisia hizo za kwa sababu ya kuwahimiza na kuwatia moyo kama wanafunzi wa kimisionari, ili wawe Kanisa linalo toka nje na kwa kuomba kutelekezwa kwa upendeleo kwa wote na kufikia maeneo ya mbali kijiografia na yaliyopo karibu, kama Yesu wa Nazareth alivyofanya.
Kanisa lipo tayari kuponesha na kambini

 

Maaskofu wa Amerika Kusini aidha wanaandika kuwa “Tunajua vizuri kwamba katikati ya ukosefu wa usawa na dhuluma ambazo bara letu linateseka, kama Kanisa daima ambalo linapaswa kubadilika lazima tutoe wito wetu wa kudumu wa uongofu ili kutambua ndoto ulizotupatia katika Wosia wa ‘Querida Amazonia’, ili kutoa nafasi kwa Kanisa ambalo linazidi kuwa Msamaria, mwenye huruma, la kisinodi, shirikishi na juu ya yote, katika huduma ya Watu wa Mungu”. Kanisa daima liko tayari kuponya majeraha kama hospitali iliyoko kambini kati ya wahamiaji, watu wasio kuwa na makazi, wale wanaosumbuka kwa vurugu, wahanga wa usafirishaji haramu na walio hatarini zaidi, ambao wananyimwa haki zao msingi, ambazo ni afya, kazi, nyumba na elimu. Kama askofu wa Roma, viongozi hawa wame sisitiza, kwamba aliwaalika watazame kwa umakini na kwa njia maalum, vijana na wazee, wanawake na watoto, watu wa asilia ambao leo hii wametengwa na kufanywa kutokuonekana na uchumi unaoua. Hatimaye, hisia za shukrani ni ile ya kuonesha njia kuu ya kuishi Injili kwa furaha na unyenyekevu wa moyo.
Makamu wa Papa:asante kushuhudia maisha

 

“Shukrani za kina na hisia za heshima na kujitoa kwa familia kwako Baba Mtakatifu Francisko ambaye katika miaka ya hivi karibuni umeliongoza Kanisa letu kwa moyo wa Ubaba. Ni maneno ya ujumbe uliotumwa na Kardinali Angelo De Donatis, makamu wa Papa wa jimbo Kuu la Roma. Kardinali, akijifanya kuwa mkalimani wa hisia za kawaida, anaonesha shukrani zake kwa Papa Fransisko na kusema “asante kwa kutufanya tugundue tena na mafundisho yako na ushuhuda wako wa maisha, furaha tamu na yenye kufariji katika kuinjilisha”.
Zawadi ya Kanisa lenye uso wa umama

 

Katika ujumbe mrefu uliosainiwa na Sr. Maria Lia Zervino, a Shirika la Mabinti wa Kanisa mjumbe wa Muungano wa Mashirika ya Wanawake Wakatoliki ulimweguni na wanamshukuru Papa Fransisko kwa kujitoa kabisa katika miaka hii 8 ya kuimarisha Kanisa. Katika ujumbe huo mrefu unarudia kufafanua zaidi kile ambacho kwa miaka hii kimeonekana kwa upande wa mafundisho na umakini wa Kanisa kuanzia familia, maskini, utunzaji wa kazi ya uumbaji, na wanashukuru sana kwa kujikita katika utetezi wa unyanyasaji uliofanywa katika Kanisa , kwa jili ya utunzaji wa majeraha ya wanawake wanaonyonywa na watumwa.“Asante zaidi ya yote kwa kujaribu kulipatia Kanisa uso wa kike unaolitambulisha kwa upole, ukaribu na huruma. Wakati huo huo kuna ombi la kuchukua hatua zaidi ambalo la kutamani kwa kina kuona faida za utajiri wa wanawake ambao ni sehemu kubwa ya Watu wa Mungu.
Kutoka Argentina picha na video

 

Mkusanyiko wa video, picha, na ujumbe ulioletwa kwa Baba Mtakatifu Francisko katika tukio la maadhimisho ya miaka nane ya upapa wake. Ni wazo ambalo limetoka chini Argentina, nchi ambayo amezaliwa Bergoglio, yaani Papa Francisko ambao umeundwa na Mtandao uitwao “Generación Francisco” kizazi cha Francisko. Kutoka kwa wahamasisha wanaandika kuwa Papa Francisko anaomba watu wote , waamini na wasio amini kusali kwa ajili yake, jitihada zetu ni kufanya hata sisi. Kuelezea upendo huo kwake ni kwa namna yak usali, na kumtakia kila la heri kwa kazi yake kubwa kwa niaba ya ulimwengu wote.