UHAI WA MAHUSIANO

Umewahi kufikiria faida zinazopatikana kwa kumkumbatia mkeo/Mumeo mkiwa mmelala? faida 6 za kukumbatiana kitandani:

1. HUPUNGUZA SHINIKIZO LA KISAIKOLOJIA:

Unapomkumbatia mkeo mkiwa mmelala husaidia kuzalisha kichocheo (homoni) cha furaha kiitwacho oxytocin. Homoni hii hufanya kazi ya kupunguza hatari ya kupatwa na maradhi ya moyo na kupunguza shinikizo la kisaikolojia. Hilo pia hupelekea kupunguza hatari ya kupatwa na maumivu ya kichwa na maradhi mengine.

2. USINGIZI MARIDHAWA:

Wanandoa wanapokumbatiana husaidia kulala vizuri. Tafiti mpya zimeonesha kuwa kumbatio hupunguza cortisol na hivyo kupunguza shinikizo la kisaikolojia. Pindi cortisol inapopungua mwilini, moja kwa moja usingizi huwa mzuri na mwanana.

3. Unapomkumbatia inaweza kusababisha raha, hasa mambo yanapofikia kwenye hatua ya kucheza, lakini kabla ya hapo furahia ladha ya mgusano wa ngozi zenu kabla ya kusonga mbele… Moyo wako unatakiwa kuuhudhurisha katika eneo na muda wa mgusano huo ili kujenga uaminifu na hisia za ushirika.

4. Kukumbatiana huwapa fursa ya kuwasiliana bila kuongea. Na hili ni jambo maridhawa kabisa kwa wanandoa kuzidi kuwa karibu.

5. NI DAWA YA FADHAA:

Kimbilia kitandani. Kumbuka kuwa kitanda kipo kwa ajili hiyo. Achana na kitabu, televisheni, simu, tablet na mambo mengine kama hayo. Kumbatio litakusaidia kumakinika na kupata utulivu.

6. HUWAPA HISIA ZA KURIDHIANA NA KUTOSHEKA:

Mnapokumbatiana bila kuwa na lengo la kuingia kwneye tendo la ndoa, mtapata hisia kubwa ya kuridhika na ndoa yenu. Tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa wanandoa wanaokumbatiana wanaridhika sana na ndoa zao kuliko wale wasiokumbatiana

Kukumbatiana ni dawa?

Sio kurupu huyu kaangalia kusini mwingine magharibi. Mnakosa tiba bora za asili?

Kukumbatiana ni kama kutumiana massage usingizi. Au Wakati wa maandalizi ya Chakula cha Usiku

??‍???‍???‍???‍???‍?
Tiba hiyo.

Na Majegero Selecius