Mhasham Baba Askofu Mkuu Beatus Kinyaia OFM Cap. Leo ameongoza Ibada ya Misa Takatifu ya Ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 10 ya utume wa Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni, Aidha Askofu Kinyaiya amepongeza juhudi za kweli zinazofanywa na mchepuo huu wa vyama vyama vya kitume , Katika mahubiri yake baba Askofu Kinyaia alitoa  mfano wa MAJI.
Maji yana viumbe wengi waishio.
Kuna viumbe hai na ambavyo sio Hai lakini pia kuna takataka nyingi pia ambazo zipo kwenye maji. (maji akimaanisha Dunia au Ulimwengu ambapo sisi tupo ndani yake.)
Lakini katika maji kuna viumbe wazuri na wabaya , Maji na viumbe wake ni kama mwanadamu na mitandao ya kijamii, mitandandao ya kijamii inaweza fanyakazi kwa kuelimisha au kupotosha jamii.
Kundi la Wamisinari Wakatoliki Mtandaoni waliona fulsa hii ya mitandao na kuamua kulipeleka huko neon la Mungu.
Takataka ni yale mengi yanayopostiwa kwenye hiyo mitandao ambayo hayana maadili katika uhai wa kiroho.
Aidha Misa hiyo Takatifu iliyoongozwa na Mhasham Baba Askofu pia ilikuwa inarushwa live (Mubashara ) na Group ya Facebook  wamisionari wakatoliki mtandaoni Pamoja na Redio Maria
Hata hiyo wamisionari waalishukuru kwa baba Aaskofu Kinyaia kwa utayari wake kuwa Askofu mweyeji wa maadhimishi hayo na pia kuwa tayari kuendesha Ibada ya misa Takatifu ya Ufunguzi.
Baada ya misa wamisionari walimkabidhi baba askofu kiasi cha Tsh 4,500,000/= kama Matendo yao ya Huruma kwa ajili ya kumsaidia baba Askofu kusomesha waseminari wanaohudumiwa na J imbo
Wamisionari wakatoliki mtandaoni pia walitumia fulsa hii kumuomba baba Askofu kuzindua kitabu cha historia ya miaka 10 ya wamisionari wakatoliki mtandaoni Tanzania katika uinjilishaji
Baada ya misa Baba mlezi wa wamisionari kitaifa baba Padre Thimoth Nyasulu Maganga alitoa neneo la shukrani
Baadae makamu mwenyekiti Taifa kwa Niaba ya Mwekiti taifa Alitoa neneo la shukrani
Pia msemaji wa wamisionari alipata muda wa kusema neneo
Misa hiyo iliongozwa kwaya ya Mwenyeheri Maria Ledochowska wa parokia ya kiwanja cha Ndege Dodoma.