Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni na wageni waalikwa leo Novemb 11, 2020 kuanza kuwasili jijini Dodoma tayari kwa ajili ya maadhimisho ya miaka kumi 10 ya utume wao.
Majimbo mbalimbali Katoliki Tanzania watashiriki Maadhimisho hayo yatakayo funguliwa rasmi kwa Misa ya Ufunguzi na Mhashamu Baba ASKOFUÂ BEATUS Â KINYAIAÂ WA JIMBO KUU KATOLIKI LA DODOMAÂ KATIKA KANISA KUU LA KIASKOFUÂ LA MTAKATIFU Â PAULO Â WAÂ MSALABAÂ 12.11.2020. (MISA ITAANZA SAA TATU ASUBUHI)
Baada ya Misa ya Ufunguzi, Kutafuatiwa na  Semina  zitakazofanyika katika ukumbi wa Kanisa la Kirutheli Karibu Kabisa na Kanisa Kuu Katoliki la Dodoma (Cathedral)
Pia katika maadhisho hayo mitandao ya kijamii ya Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni inayofanya shughuli za uinjilishaji itazinduliwa rasmi.
Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni wanatumia mitandao ifuatayo katika kusafirisha ujumbe wa Neno la Mungu.
1.Facebook Group – WAMISIONARI WAKATOLIKI MTANDAONI
2.Facebook Page – Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni
3.Istagram – Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni
4.Twitter –Â Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni
5.Telegram – WAMISIONARI WAKATOLIKI MTANDAONI
- Website:Â Â www.wamisionariwakatoliki.or.tz
Pamoja na tukio hilo pia kutakua na tukio la kuzindua Kitabu cha Historia cha Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni Tanzania Kilichoandikwa na Mwandishi na Mahiri WILLIAM BHOKE
Wamisionari wanawakaribisha katika semina zitakazo endeshwa na
Padre Titus Amigu – MADA YA SAKRAMENTI YA UPONYAJI
Padre Joseph Mosha – UMISIONARI NA UTUME WA VIJANA KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII
Fr Stephen Kadilo – AFYA NA MALEZI YA VIJANA
Mr Prosper  Magali – MBINU ZA KUKUZA,KUANZISHA BIASHARA (UJASILIAMALI)
Kuanzia tarehe 12 – 13.11.2020
Tarehe 14.11.2020 Itakuwa kilele cha Maadhimisho haya ambayo misa Takatifu na Shughuli mbalimbali
Zitaendelea katika kanisa kuu la Kiaskofu Jimbo kuu la Katoliki la Dodoma na Baadae Sherehe ya Kilele katika ukumbi wa SANTHOME WA SHULE YA MASISTA WAABUDUO EKARISTI
MATANGAZO YA MISA YA UFUNGUZI NA YA KILELE YATARUSHA NA REDIO MARIA TANZANIA LIVE
PI BAADHI YA MITANDAO YA KIJAMII INAYOTUMIKA NA WAMISIONARI HAO MTANDAONI YATARUSHA MADAÂ NA MATUKIO LIVE.
Imeandaliwa na Mwenyekiti Wa Kamati ya Mitandao Kitaifa ( Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni) Majegero Selecius, Edited by Nicolaus