Isaya 6:8 Mimi hapa nitume Bwana”

UTUME wa Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni, ukiongozwa na Baba Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Jude Thaddaeus Ruwa’ichi akishirikiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma, Beatus Kinyaia unawakaribisha waamini WOTE wa Jimbo Kuu la Dodoma pamoja na waamini wa majimbo mengine yote katika SHEREHE YA KUTIMIZA MIAKA 10 ya utume wetu yatakayofanyika kuanzia tarehe Novemba 12 hadi Novemba 14,  2020.

 

Misa ya ufunguzi itafanyika tarehe 12/11/2020 kuanzia saa 3:00 asubuhi kanisa kuu la Mtakatifu Paulo Msalaba na itaendeshwa na Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya.

 

Baada ya hapo zitafuta mada mbalimbali zitazofanyika kwenye ukumbi wa Kanisa la Kilutheri Dodoma na zitakazoongozwa na wafuatao

Watakaotafakarisha:-

1. Padre Titus Amigu: ” * Sakramenti na uponyaji “

2. Pd Joseph Mosha: ” Umisionari na utume wa vijana kupitia mitandao ya kijamii

3. Mmsionari Prosper Magali Mbinu za kuanzisha,kukuza, na kuendeleza miradi/biashara

4. Pd Dr Stephen Nyakumosa Kadilo: ” Afya na malezi ya vijana

Watakaotuongoza katika kumwimbia MUNGU ni kwaya za:
1. Kwaya ya Maria Leodekosika
2. Na kwaya ya Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni.

Siku ya tarehe 14.11.2020 kilele cha Sherehe tutahitimishwa kwa ibada ya Misa takatifu itakayoongozwa na Askofu Mkuu Mhashamu Beatus Kinyaiya, kwenye Ukumbi wa Santhome Nkuhungu Jimbo kuu la DODOMA

VIONGOZI WOTE WA VYAMA VYA KITUME WANAOMBWA KUSHIRIKI.

KILA PAROKIA IHAKIKISHE INATOA WATU WA KUTOSHA KWANI WATAPATA WASAA WA KUJIFUNZA MAMBO MBALIMBALI YATAKAYOKUZA IMANI YAO

NI MAADHIMISHO MUHIMU SANA.
KARIBUNI

Kwa mawasiliano Zaidi piga namba zifuatazo

-0713 260249

-0763 787575

-0621 038790