Umisionari ni dhamana na wito wa Kristo Yesu kwa wabatizwa wote. Kila mtu anapaswa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu kadiri ya nafasi na mazingira yake. (AFP or licensors)

Padre Adolf Bernard Minga, Mratibu wa Utume wa Vijana, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC, hivi karibuni ameendesha semina kwa vijana wa kizazi kipya kutoka Parokia ya Kambikatoto Jimbo kuu la Mbeya, Tanzania. Amekazia umuhimu wa kunafsisha dhana ya umisionari katika kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu; Maisha ya sadaka na Mazingira ya dhambi za ujana.

Na Padre Dr. Adolf Bernard Minga, – Mbeya, Tanzania.

Tangu ujio wa pili wa Vatikano Kanisa katoliki limepitia mabadiliko mengi sana yanayo weza kulinganishwa “hewa mpya ndani ya chumba” wengine walikejeli kama ni “vurugu” kama kawaida ya binadamu tulivyo.Ukichunguza kwa makini utagunduwa kwamba mabadiliko hayo yalilenga kuleta uhai ndani ya Kanisa na pia kuwashirikisha walei au wanafamilia katika maisha ya wokovu wa dunia nzima ambayo kwayo ndilo lengo la umisionari “nimekuja ili wawe na uhai ,wawe nao tele,sakramenti ya wokovu kwa wote” (LG 48). Maisha ya Kisakramenti.  Ili kuita Kanisa mambo matatu ni ya msingi mno: Neno la Mungu; Maisha ya Sakrame na Maisha ya Jumuiya. Katika Kanisa asilimia zaidi ya 99% ni waamini walei hivyo ni waamini hai na washiriki wakubwa wa Taifa la Mungu.  Walei mnayo nafasi kubwa na muhimu na ndilo kundi kubwa kuliko kundi la wakleri na watawa.  Walei wanashiriki katika: Kutoa ushuhuda wa kikristu- Mnaishi maisha ya jumuiya, mnaelewa mila zenu ila cha pekee ziendane na mwanga wa Injili. Ushuhuda wa kikristo unapaswa kuwa kwanza ni ushuhuda wa mapendo ya Mungu (Yohane 11:11) na kidugu bila kuchagua. Lazima mshiriki katika kuleta maendeleo ya kweli kama uchumi bora, maisha mema ya jamii, elimu kwa wote, mna kazi ya kushiriki wokovu kwa wote.

Kuhubiri na kushuhudia Injili. Kazi hii si ya wakleri tu bali ya ya wote. Sisi sote tu wamisionari. Tuhubiri Injili kwa midomo na matendo mema chini ya Uongozi wa Roho Mtakatifu. Ni vizuri kushiriki kuwandaa Wakatekumeni kwa kuchunguza nia zao, kuelekeza na kuwaingiza hatua kwa hatua kama unyago wa kweli wa kikiristu, katika maisha ya kikristo. Kujenga jumuiya ya kikristo walei watambue kwamba kazi misioni siyo tu kutoa ushuhuda wa kikristo na kuhubiri Injili, bali pia kujenga familia ya Mungu, Taifa la Mungu. Niseme tu msingi wa Sakramenti zote ni neno la Mungu, siku ya ubatizo hata kama tutamwagia mtu pipa zima la maji bila kuelewa unafanyiwa nini ni bure.  Unamkataa shetan? Humjui, na mambo yake huyajui? Nguruwe ukimwogesha anaangalia yale maji yenye uchafu yanaenda wapi?

Umisionari wenyewe ni kutumwa: Makundi yanayopaswa kuinjilishwa: Ni wale wote wasiomjua Mungu kwa njia ya matendo ya huruma bila ubaguzi- mfano unamjengea mtu nyumba baadaye anashangaaaa. Wanaomjua Mungu bali wamelegea, hawa wanahitaji uinjilishaji mpya unaofumbatwa katika ushuhuda na Semina mbali mbali. Wale waliokata tamaa waszaidiwe na Jumuiya ndogo ndogo za Kikristo. Walio katika mazingira magumu na hatarishi suluhu ni huduma msingi za jamii kama vile: shule, hospitali na miradi ya maendeleo fungamani ya binadamu. Uinjilishaji uliofanikiwa na endelevu ambao hatimaye umekuwa mti mkubwa na wa faraja, tukumbuke kuwa kulikuwa na majaribio mawili kabla na ambayo hayakufanikiwa. Kwanza na mapadre Kireno kwenye karne ya 14 wakiwahudimia zaidi wasafiri wa baharini. Baadaye kwenye Karne ya 16 walikuja mapadre Waagustini ambao baada ya kipindi kifupi walifukuzwa na utawala wa Kiislamu na hata wengine kuuwawa. Hatimaye walikuja Mapadre kutoka Kisiwa cha Reunion waliotumwa na Askofu Rene Maupoint mwaka 1860.

Na miaka mitatu baadaye Askofu huyu aliona kazi kubwa ya uinjilishaji mbele yake na uwezo mdogo wa jimbo lake na hivyo akaomba uongozi wa Kanisa Roma ukabidhi utume huu mkubwa na muhimu kwa Shirika lenye uzoefu na lenye uwezo wa watenda kazi la Mapadre na Mabruda wa Roho Mtakatifu. Hawa walifika mwaka 1863 na kwa miaka mitano waliishi na kufanya kazi Zanziba kabla ya kuja bara kupitia Bagamoyo mwaka 1868. Hata baada ya miaka 150 bado yapo mengi ambayo tunaweza kujifunza kutoka kwa hawa wamisionari na hata kuwa majibu kwa changamoto tunazokabiliana nazo za karne yetu ya 21: Tujifunze nini kutoka kwa wamisionari wa mwanzo na Kwa Imani yao. Umuhimu wa kusoma alama za nyakati kwa usahihi: Askofu Rene Maupoint na Mapadre wake waliona ugumu wa utume wenyewe pale zanziba na maeneo ya bara (lugha, mazingira, watu na desturi tofauti); uzoefu wao mdogo (walikuwa Askofu na mapadre wa Jimbo) na ukubwa wa utume huo (kuinjilisha Afrika ya Mashariki na kati) hata hivyo kusukumwa kutafuta na kukabidhi kazi hii kwa watu wengine wakitambua kuwa ilikuwa kazi ya Mungu na mwisho wa siku hajalishi ni nani anaifanya (Rej. 1 Kor. 1:10-15).

Nao Mapadre na Mabruda wa Shirika la Roho Mtakatifu walikuwa makini kusoma alama za nyakati na hii ilikuwa moja ya nguzo kubwa za mafanikio yao ya kazi ya uinjilishaji wa kina. Mara walipofika walitambua kuwa bila mahusiano mazuri na utawala wa kiislamu wasingeweza kufanya chochote. Kwa maneno mengine, walitambua kuwa kwa kadiri watakavyokaribishwa na kukubalika na uongozi wa wakati huo ndio hivyo matumaini ya ufanisi wa utume wao yangeongezeka. Ndio sababu siku moja baada ya kufika zanziba walikwenda kumtembelea Sultani Seid Majjid na toka siku hiyo ukazaliwa uhusiano wa karibu sana na hata Sultani kutamani uwe wa kindugu! Alama za nyakati ziliwaelekeza pia kutambua kuwa uinjilishaji ufanyike kwa kuwa jibu la tatizo la wakati huo, hata kama ni kwa kiasi kidogo: tatizo la biashara ya utumwa na hivyo kuwarudishia utu na uhai wale watumwa ambao walikuwa hawana tena thamani hata ya kuwa mtumwa kwa mabwana wao. Kwani hata kwenye soko la watumwa walikuwa wamepoteza thamani ya kuuzwa au katika nyumba za mabwana wao walikuwa hawana faida tena bali hasara.

Uinilishaji wowote ambao ni wa mafanikio na ni endelevu ni lazima uwe ule uliosoma alama za nyakati na kuzielewa vyema kwani ni kama maelekezo kutoka kwa Roho Mtakatifu na maagizo ya Kristo Yesu, Bwana ma Mwokozi wa wanadamu. Ndio sababu leo hii tunakumbushwa na kuzungumza juu ya umuhimu wa Uinjilishaji Mpya (New Evangelization and Re-evangelization).  Leo hii tufikiri kuhusu Jumuiya Ndogo ndogo za Kikristo zikoje?  Moyo wa kujitoa bila kujibakiza: Tukumbuke hawa wamisionari waliokuja kwetu kutuinjilisha wakifuata mfano wa baba yetu wa imani Ibrahimu (Mwa 12:1). Waliacha yote huko kwao na wakajivika silaha ya Imani iliyojikita kwenye Neno la Mungu au Habari njema kwao na kwa wale watakaowainjilisha. Hawakujali umri wao mdogo, uzoefu wao au ugumu wa utume wanaoitiwa.  Wengine walikuwa na umri mdogo wa miaka 27 tu lakini cha msingi na muuhimu ni kwamba waliamini kwamba kuitwa na Mungu ni jambo la kipekee na lenye heri na kuitikia ni faraja kubwa. Moyo huu wa sadaka na matoleo bado unahitajika sana katika karne hii yetu ya 21. Tujifunze kujisahau, kujitoa na kuwafikiria wengine kwani huko ndiko kwenye hazina na malipizi ya kudumu. Moyo huu wa sadaka na matoleo ya wamisionari hawa havitasahaulika na cha muhimu zaidi ni kwamba majina yao yameandikwa mbinguni.

Kanisa la hapa duniani, sisi Kanisa la wasafiri tutawakumbuka daima kwa moyo wa shukrani kwa Mungu na kwao na watabakia taa ya kuangaza hatua zetu na mfano bora wa kuigwa. Umuhimu wa kuwa na mahusiano mema na viongozi wa wakati uliopo. Kama binadamu hatukuumbwa kama visiwa. Binadamu ameumbwa ili awe na mahusiano na wengine, hasa na wale waliokabidhiwa jukumu la uongozi. Inawezekana hata wakawa ni viongozi ambao hawakidhi matarajio yetu. (Padre Antony Horner alitamani sana kama Sultani aliyekwenda kumtembelea kwenye makao yake angekuwa mkatoliki lakini alikuwa ni wa dini nyingine). Hata hivyo alitambua kuwa kazi yake ya Kikristo isingefanikiwa kama asingekuwa na uhusiano mzuri na yeye. Pia tunaona wamisionari hawa walipokuja kuinjilisha Tanzania bara na kwingineko walijitahidi kwanza kuwa na uhusiano mzuri na Machifu au viongozi wa makabila mbali mbali na pale uhusiano ulipokuwa mzuri ulizaa matunda mengi kwenye kazi yao ya uinjilishaji; ulizaa matunda bora na ya kudumu. Uhusiano huu ulielekezwa hata kwa wakristu wa madhehebu mengine.

Wamisionari walichukua kazi ya Uinjilishaji kama kazi ya Kanisa na wala siyo kazi ya mtu (mmoja) binafsi au kikundi kimoja au Shirika moja. Ndio sababu kazi hii iliendelea hata pale baadhi yao walipofariki au ilipobidi kuondoka wa ajili ya utume mwingine. Na ndio sababu tunawaona hata mapadre wa Shirika la Roho Mtakatifu wakiwapokea kwa furaha mapadre wa mashirika mengine (Wamisionari wa Afrika na Wabenediktini) waliofika Bagamoyo baada yao na hata kuwaandalia safari ya kuingia bara na kuwapatia wasaidizi walioandaliwa vyema kuandamana nao. Kulikuwa hamna roho ya ubinafsi na ya ushindani wakitambua tu kwamba sifa na utukufu vilikuwa kwa Mungu peke yake na siyo kwa mtu, kikundi au Shirika. Leo hii licha ya utandawazi bado tunasikia lugha ya ‘kazi yangu’, ‘kazi yetu’, ‘kazi ya Shirika langu’, halafu parokia/shule/ yangu, chuo chetu n.k. Ni kwa kiasi gani tunauona utume wetu kwa mapana na kwa kina zaidi? Tukumbuke kuwa tunachokifanya ni sehemu ndogo sana ya Kazi ya Kanisa na Kazi ya Mungu ya kuukomboa ulimwengu. Umuhimu wa kutegemeza Kanisa mahalia kabla ya kujitegemeza mwenyewe.

Tutambue nia ya pekee ya wamisionari hawa ilikuwa kuanzisha na kulitegemeza kanisa mahalia na kuliwezesha kujitegemea kwa kuwaandaa watenda kazi wazawa na kuwa na miradi ya kuendeleza kazi waliyoianzisha. Ndio sababu wamisionari wa shirika la Roho Mtakatifu walianza kwanza kuandaa Makatekista wa kuwasaidia katika kazi ya uinjilishaji mwaka 1877 na kuanzisha seminari kwa ajili ya kuwaandaa mapadre wazawa ya Mt. Yakobo, Kilema mwaka 1926 na Kibosho mwaka 1940. Hata jitihada zilizoanziswa mapema zaidi kule Zanzibar na Bagamoyo zilikuwa ni kwa ajili ya kupata watenda kazi wa kanisa mahalia. Shirika hili lilianza kukubali na kuandaa vijana kwa ajili ya Shirika lake zaidi ya miaka 100 tangu lifike Tanzania! Kwani walifika mwaka 1863 na padre wao wa kwanza alipata upadre mwaka 1977! Kujifikiria wenyewe na mahitaji ya Shirika yalifuata baadaye na baada tu ya kutimiza nia yao ya kwanza. Siku hizi hali inaonesha kuwa kuna makundi ya dini hata ya kikatoliki ambayo yanakuja na nia hii ya pili kwa sababu ya hali ya huko yanakotoka. Sana sana nia hizi mbili zinakwenda sambamba.

Wamisionari wa kwanza walipokuja na baada ya kuinjilisha kwa muda na utume kushamiri na kuwa mkubwa na unaohitaji wafanyakazi wengi zaidi waliwandaa wazawa kwa ajili ya utume huu na siyo kwa ajili ya Mashirika yao. Pia walijenga makanisa, mashule, mahospitali na miradi mingineyo ambayo haikuwa ni kwa ajili ya Mashirika yao. Kwa hili tuna mengi ya kujifunza na hasa mashirika yanayokuja kwetu leo hii. Kwani roho ya kujenga na kutegemeza Kanisa mahalia haionekani inavyostahili, angalao kwa baadhi yao na hivyo kutufanya tujiulize utume unaofanywa ni kwa ajili ya nani? Kweli ni kwa ajili ya sifa na utukufu wa Mungu? Wamisionari walitafuta kumkomboa na kumwinjilisha mtu kwa kila hali. Wamisionari waliotuletea Injili hawakujenga tu makanisa bali pia shule za kufundisha maarifa na za kufundisha ufundi stadi, vituo vya afya ili kutupatia maarifa na afya, vitu muhimu kwa miili yetu na maendeleo ya jamii nzima. Pia walileta na kuotesha mazao mbalimbali ya chakula na biashara. Walitambua kuwa matatizo yanayomkabili mwanadamu hayana njia za mkato bali yanahitaji uwekezaji thabiti na mpana na ambao ni endelevu.

Zama hizi zetu tunapaswa kujikumbusha hili na kufuata nyayo za wamisionari hawa waliotuletea Habari Njema ya Wokovu; kwani kishawishi cha kutumia njia za mkato kwa changamoto za msingi zinazomkumba mwanadamu wa leo hii kama magonjwa ya mwili na akili na hata ya kiroho kimeongezeka hata kwa wale wanaomfahamu Kristo. Wamisionari waliotuletea Injili miaka 150 iliyopita walikuwa ni watu walioaaminika na watu wote na kuwa wapatanishi wa wote. Tukumbuke kuwa walipokuja ulikuwa ni wakati wa vita kati ya makabila na makabila na wakati mwingine ilikuwa hata ni vita kati ya waafrika (wazawa) na wakoloni (wageni na watawala) na ilikuwa si rahisi kuwatofautisha wamisionari hawa na wakoloni ambao walionekana kama ndugu zao kwani hata walikuwa na rangi moja (nyeupe). Lakini hamna wakati walitiliwa shaka au kuonekana ni wasaliti. Badala yake walitumiwa na pande zote (wazawa na ndugu zao wakoloni) kama Wapatanishi waadilifu na wanaotenda haki kwa wote na ambao daima walitambua thamani ya amani na udugu wa binadamu wote kama watoto wa Mungu.

Inakuwaje leo hii kwamba damu, kabila, lugha, rangi, cheo, jinsia vinapewa kipaumbele zaidi ya imani yetu kwa Kristo na hivyo kufifisha ule mwanga tulioupokea siku ile ya ubatizo? Kuwa wapatanishi na wanaoleta amani siyo vitu vya ziada bali ni tunu muhimu katika wito wetu (Rej. Mat. 5:9) kwani vinatufanya watoto wa Mungu, ndugu zake Kristo, Mfalme wa Amani; na Hekalu ya Roho Mtakatifu, Mpatanishi na Mleta Amani. Tujifunze kutowahukumu Wamisionari hawa au namna walivyofanya utume wao zama zao kwa kutumia ufahamu wetu na nyenzo za sasa. Kwa mfano tunaweza kuhoji ni kwa nini walikwenda kama wanunuzi wengine kwenye soko la watumwa na kunua watumwa au busara ya kuinjilisha na kujenga kanisa la Afrika Mashariki kwa kuwatumia watumwa waliowanunua na kuwarudishi uhuru na utu wao.  Je; nia hii haikuwa kipingamizi cha kuwainjilisha waafrika wengi ambao walikuwa hawajaonja hali na machungu ya kuwa mtumwa? Tunapaswa kutambu kuwa Mapadre hawa walikabiliana na hali walivyoikuta na kuwa wakweli na, kwa kiasi kikubwa walifanikiwa katika utume wao na hivyo kufanya kazi yao kuwa ya mafanikio.

Hivyo kutumia ufahamu wetu wa leo na nyenzo tulizonazo kuwahukumu siyo haki hata kidogo. Badala yake, tutambue kwamba walijitoa kabisa kwa Mungu na kazi yake na hiii ilifanya utume wao uwe zaburi kwa vizazi vijavyo na hivyo kwamba hatimaye wote tutaimba Aluleya kwa Mungu aliye juu. Kwani pamoja na yote, wamisionari hawa wametuachia urithi usiosahaulika kwa jamii yetu ya leo na ijayo; urithi ambao bado unaendelea kuwa chachu kwa Kanisa na jamiii ya leo. Haya ndiyo machache kati ya mengi ambayo tunaweza na tunapaswa kujifunza kutoka kwa wamisionari waliotuletea Injili na utendaji wao. Lakini pia hii itakuwa namna ya kuenzi miamba hii ya imani katoliki. Na mwisho itakuwa ni namna ya kuendeleza kwa ufanisi kazi ya Ukombozi wa kwa kizazi chetu na vizazi vijavyo.

Swali la kujiuliza hapa Kambikatoto ni Mazingira gani yanayotuingiza zaidi kwenye dhambi’? Kiburi: Mtu anajiona ni zaidi ya wengine au chama kimoja cha kitume kinajiona ndo kila kitu parokiani. Mtu mwenye kiburi haoni wengine kama wanajua.  Anajiona anajua majibu ya maswali yote. Unyenyekevu ni kutambua kwamba kuna vitu naviweza na vitu vingine siviwezi. “Kichwa cha mtu ni kichaka” kwa maana kwamba huwezi kujua mtu anafikiri nini. Watu wengine wanajua Kuhusu wewe ila wewe hujui. Wewe hujui na mtu mwengine naye hajui. Mfano leo hii kujua ni lini watu watasema wewe ni mwema ni vigumu kujua. Cha msingi ni unyenyekevu na kuruhusu kujifunza toka kwa wengine.  Kiburi kinatuingiza katika dhambi na hivyo hata kumkataa mwenyezi Mungu.

Choyo: Ni kufurahia mali na kukumbatia mali hata kama huvitumii au huvihitaji. Ukusanyaji wa vitu visivyokuwa na mpango. Tamaa za MwiliMwili unapenda kuridhisha tama zake. Kwa kawaida mwili unataka.  Mwili unapenda kusikia mapishi ya tamaa. Hiyo ndo asili yenyewe. Kitu asilia twajua sote. Unavutiwa na mtu unahitimisha ananipenda. Unapanga utekelezaji.  Mantiki kuhitimisha mambo haifai. Wivu: Ni pale ambapo mtu anasikitika kwa mafanikio ya wengi.  Unasikitika kila mtu anaona.  Mafanikio ya wenzetu iwe changamoto yetu. Ulafi: Kufurahia kula na kunywa bila kuwajali watu wengine. Mtu hawajali wengine.  Mtu anataka wengine wasile chakula ale yeye. Hasira: Wanawake wanaairisha hasira, ukimwambia nisamehe ansema nimekusamehe, rudia utaona. Wakati wanaume wanatawaliwa na hasira hawasamehi kirahisi. Uvivu; Tabia ya kutopenda kufanya kazi kuendeleza umbeya, kulala lala tu.Usuda na kijicho! Tunakeleketwa, tunakuwa na masikitiko  na chema cha mtu mwingine.

URAFIKI. Rafiki ni mtu unaye mwamini na yuko tayari kuumia kwa ajili yako, unajifunua kwake. Kwa urafiki, Mtu anatafuta usalama- kumshirikisha mengi. Katika urafiki tunatafuta Amani. Katika Urafiki kikubwa tunachotafuta ni furaha. Watu wanalia sababuKuna urafiki wa kusalitianaKuna urafiki wa kudanganyanaKuna urafiki wa kuwa chamboKuna urafiki ambao hamtunziani siri. Kuna urafiki wa kutafuta faida tu. Urafiki wa binadamu una hira na mapungufuUrafiki wa kweli tunapata wapi? Rafiki wa kwanza ni Yesu usalama wa mwisho na amani ya mwisho ni Yesu. Penda wote lakini Rafiki ni Yesu.  Rafiki hata wa ndoa zenu ni Yesu. Urafiki wa kidunia una makovu mengi. Moyo ukiwa mtupu utatafuta rafiki moyo ujazwe na Yesu.

KUMPENDA YESU MAANA YAKE NINI? Tunaweza kuwa Wakristu wa siku nyingi lakini bado hatujampenda Yesu. Fikiri humpendi Yesu halafu kila mara uko kanisani kwa ajili ya nini sasa? Wengi wanaitwa kwa ubatizo lakini ni wachache sana wanaitikia mwitikio huo, wachache waaminifu na wachache wanampenda Yesu.Upendo maana yake unaweza kuufia, yaani ni hatua ya juu sana unaapoongelea upendo. Mapendo yoyote kuyajenga ni kazi. Usikurupuke.

YESU ALIWEKA SIFA ZA KUMPENDA: Yohane, Maria mke wa Kleopa na Maria Mama yake na Maria Magdalena- Ndio waliojitoa kwa Yesu mpaka Msalabani.  Padri mmoja na Wawata watatuTukue katika mapendo yetu kwa Yesu. Mtu akinipendaAtalishika Neno langu na Baba atampenda nasi tutakuja kukaa kwake Yn 14:23 na kukaa naye. Penda bila kikomo samehe bila kukoma.  Mshindi katika upendo, ushindi katika kusamehe, hilo ndilo neno la Yesu kwa Ufupi. Penda kukaa na Yesu na kuongea na YesuUnayempenda utatenga muda kwa ajili yake Utajisikiaje unafika kwa mtu anakufungulia TV alafu anaondoka. Watu wengine ni viongozi wakubwa lakini bado wana muda na Yesu.

Mt. Thomas Aquinas “Napata hekima toka kwa mwenye hekima- Asubuhi mpaka jioni. Kutoa tu haitoshi, tukae pamoja. Mshirikishe, jifunue, Tabernacle wengine wanachukulia kama ni Friji. Lk 9: 13, Mtu akitaka kunifuata ni sharti ajikane nafsi yake ajitwike Msalaba. Kujikana Kumpa Kristo Yesu enzi katika maisha yako, katika makasoro yako zuia ili uwe karibu na Kristu, Jidhibiti na Jimiliki. Sio kujikana tu beba Msalaba, yaani stahimili magumu yote unayoyapata maishani. Kujitoa kwa wengine. Jitoe kwa utumishi kwa ajili ya wengine. Petro anaambiwa tunza kondoo wangu. Tumtumikie Yesu sio kinadharia bali kimatendo. Vijana mjitambue ninyi ni nguzo ya Kanisa hivyo kuweni mashuhuda wa imani, sala  na usomaji na tafakari ya Neno la Mungu