Vyombo vya Habari Katoliki,vimewekwa ili kukabiliana na changamoto za ulimwengu mamboleo unaothamini zaidi habari za kiulimwengu.Kanisa linaishi ili kutimiza utume wake wa kiimani.Ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu,Panama na Rais wa Baraza la Ushauri la vyombo vya Mawasiliano Katoliki,akivishukuru kwa kuwa vimekuwa kiunganishi katika kipindi cha karantini na mchango katika kuwaunganisha wananchi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Askofu Manuel Manuel Ochogavía Barahona, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu la Panama na Rais wa Baraza la Ushauri la vyombo vya Mawasiliano Katoliki,Panama amevishukuru vyombo vya habari ambavyo vimekuwa kiunganishi katika kipindi cha kujitenga,na vimetoa mchango mkubwa katika kuwaunganisha wananchi.

Kanisa linaishi ili kutimiza utume wake wa kiimani

Akitoa shukrani zake za dhati, amevishukuru vyombo vya habari na kwa namna ya pekee kwa kazi za waandishi vilivyowavusha watu katika janga la virusi vya Corona na kudumisha umoja wa waamini. Askofu Ochogavía Barahona ametoa ujumbe huu kuhusu Vyombo vya Habari Katoliki, ambavyo vimewekwa ili kukabiliana na changamoto za ulimwengu mamboleo unaothamini zaidi habari za kiulimwengu. Kanisa linaishi ili kutimiza utume wake wa kiimani.  Askofu amefananua kuwa Kanisa la Ulaya leo hii lina Parokia nyingi zimejiunga na uinjilisha wa kimtandao wa kidijitali. Huo ni utajiri mkubwa.

Uinjilishaji unaofanywa na vyombo vya habari uyafikie makundi yote katika jamii

Vyombo vya habari, ni mchango mkubwa katika kuwasaidia waamini kuishi maisha ya Ekaristi Takatifu kwa njia ya sala, usomaji wa Maandiko Matakatifu, ufuatiliaji wa wosia wa Papa Francisko kwa Jumuiya nyingi za Panama. “Hakuna aliye na furaha zaidi, kwani kuna mengi bado ya kufanya” amefafanua Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu.  “Uinjilishaji unaofanywa na vyombo vya habari unapaswa kuyafikia makundi yote katika jamii. Ili kufikia hatua hii muda unahitajika bado wa kujifunza mengi.

Kila jambo linahitaji kujitolea na kuwekewa misingi madhubuti yenye misingi ya kiubatizo

Akihitimisha Askofu Ochogavía katika kuwasilisha ujumbe wake amesema, kila jambo linahitaji kujitolea na kuwekewa misingi madhubuti yenye misingi ya kiubatizo na ya kiumisionari. Kama injili invyotudai, kwenda ulimwenguni kote kuihubiri habari njema. Kadhalika amewasisitiza wanahabari kuandaa vema habari zao ili kufikisha ujumbe mahususi kwa jamii tarajiwa. Aidha, ameviomba vyombo vya habari kuendelea kujenga utamaduni wa kuwaaunganisha watu na hasa kipindi hiki ambacho baadhi ya makanisa bado yamefungwa.