Na Sr. Angela Rwezaula;-Vatican.
Dominika tarehe 2 Agosti ni Siku ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar Secam iliyotangazwa mnano mwaka 2014, wakati wa fursa ya miaka 45 tangu kuanzishwa kwa chombo hiki ambacho kinaleta pamoja Mabaraza ya maaskofu kitaifa 37, na mabaraza 8 ya kanda za Afrika. Siku hiyo uadhimishwa kila tarehe 29 Julai au ikiwa haiendani na Dominika iliyo karibu sana na basi inaweza kusongezwa kwa maana hiyo mwaka huu imeangukia Dominika ya tarehe 2 Agosti.
Fursa ya wakatoliki wa Afrika kujua shirikisho hili na utume wake kwa Kanisa
Siku hiyo imekusudiwa kuwa fursa ya kuwafanya Wakatoliki wa Kiafrika ili wajue historia, uundaji wa chombo hiki na utume wa shirikisho hilo lakini pia kwa ajili ya kuliombea Kanisa la Ulimwenguni na kwa namna ya pekee barani Afrika. Kwa kawaida siku hiyo uambatana na makusanyo maalum, lakini kwa sababu ya dharura ya virusi vya corona mwaka huu kwa taarifa ya barua kutoka kwa Katibu mkuu, Padre Terwase Henry Akaabiam, iliyenukuliwa katika blogi ya Mabaraza ya Maakofu wa Afrika Mashariki ya (AMECEA)kwamba makusanyo hayo yameharishwa. Lakini Padre Akaabian amebainisha katika brua yake iliyoelekezwa kwa makatibu wakuu wa Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika kwa kuwa wale ambao wanataka kutoa mchango wa kifedha au vitu wanaweza kufanya hivyo.
Secam iliundwa mwaka 1969
Makusanyo hayo husaidia kuunga mkono kazi na utume wa Secam na ni njia ya kuwafanya Wakatoliki wote wa Kiafrika ambao ni washiriki kamili kuhisi kuwa sehemu yake ameeleza Padre Anthony Makunde, katibu mkuu wa Amecea. Kunako mwaka 2019 Secam ilifanya sherehe za Jubileo ya dhahabu. Shirikisho hili liliundwa kunako mwaka 1969 na kuzinduliwa na Papa Paulo VI kunako mwezi Julai mwaka huo huo katika fursa ya ziara yake ya kitume nchini Uganda, ikiwa ni kwa mara ya kwanza Papa katika Bara la Afrika.
Kudumisha na kuhamasisha ushirikiano kidugu
Wazo la kuunda muundo wa bara lenye uwezo wa kukuza maono ya pamja ya utume wa Kanisa barani Afrika, lilikomaa mara baada ya Mtagusi wa II wa Vatican, wakati maaskofu wa Kiafrika walionyesha mapenzi yao ya kutenda kwa muungano,kwa kushinda tofauti za lugha zao, kihistoria, na kitamaduni. Lengo kuu maalum la Secama kwa maana hiyo ni kudumisha na kuhamasisha ushirikiano wa kidugu na ushirikiano wa Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika, hasa katika kujikita na mahusiano ya uwanja wa uinjilishaji, haki na amani na mazungumzo ya kidini.