Wamisionari wakiwa Nje kabla ya kuonana na Baba Askofu Mkuu

Mungu Mwenyezi,Baba wa milele, ni wewe unayemwita kila mtu akutumikie na akufikie wewe kadiri ya wito uliomjalia.
Ni wewe unayemtaka kila mmoja apate ukamilifu katika wito wake.
Tunakushukuru kwa wito wa Umisionari mtandaoni uliotuitia,na tunakushukuru kwa kuwa nasi kwa kipindi cha miaka kumi (10) ya umisionari mtandaoni.
Tunaomba nguvu zako,ili kweli tuwe Wamisionari hodari wa mtandaoni,ili tuweze kuwainjilisha na kuwaleta watu wengi kwako,ili wakujue,wakupende na wakutumikie kwa njia ya mitandao na mwisho wapate kufika kwako juu Mbinguni.
Tunakuomba,utujalie tuwe kweli chumvi kwa wenzetu,tuwe mwanga na njia ya kuwaongoza wenzetu katika kutumia mitandao ya kijamii, katika kukutafuta na kukutumikia wewe Mungu wa kweli,na Mungu wa milele.
Baba,tunakuomba uwabariki viongozi wetu wanao tuongoza. Ubariki juhudi na majitoleo ya kila mmoja wetu,na ubariki maisha yetu pia.
Tupe nguvu na busara ya kupambana kwa ujasiri dhidi ya muovu shetani,ili utume wetu uzidi kuimarika na kutoa matunda yaliyo bora.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu…
AMINA.

Maria Mtakatifu mkingiwa dhambi ya asili na mwombezi wa mataifa yote..utuombee

Baba yetu…
Salamu Maria…
Atukuzwe Baba…