Papa Francisco, leo Mei 13, 2020 amemteua Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Eusebius Alfred Nzigilwa, kuwa akofu mpya wa Jimbo la Mpanda
Januari 28, 2010 alitangazwa na Papa Benedicto XVI kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam
Askofu Nzigilwa anachukua nafasi iliyoachwa na Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga baada ya kuhamishiwa Jimbo Kuu la Mbeya mwaka 2019
Askofu Eusebius Alfred Nzigilwa alizaliwa Agost 14 1966 Mkoani Mwanza. Alipewa daraja la Ushemasi Januari 6, 1995, alipewa upadrisho Juni 23, 1995 na Askofu Mkuu Polycarp Pengo.