Waziri wa Katiba na Sheria , Balozi Dkt Augustine Mahiga amefariki dunia alfajiri ya leo Mei 1, 2020 baada ya kuugua ghafla akiwa mjini Dodoma.

 

Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi na kumuelezea Balozi Mahiga kuwa ni mchapakazi, mzalendo na mwanadiplomasia mahiri.