Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican
Maisha ya milioni ya watu, katika ulimwengu ambao tayari unachangamotishwa na matatizo mengi ya kukabiliana nayo na zaidi kwa ajili ya janga hili, yamebadilika na kuweka majaribu magumu. Watu wadhaifu zaidi, wasioonekana, watu wasio kuwa na makazi, wanaohatarisha kulipa gharama nzito zaidi. Hawa siyo karatasi rahisi lakini ni ishara ya utu uliopatikana tena, ya ukombozi uliopatikana na shukrani kwa kazi ambayo inafanyika bila kuonekana zaidi. Ni sauti ambayo haina usawa kwa sababu ni kwikwi au kilio cha hali isiyo na usawa. Ni historia ya wauza magazeti zaidi ya 100 ya barabarani ambao Papa Francis anawaelekeza, kwa barua yake, akiwaita kuwa ni watu”wa kushangaza”, huku akiwatia moyo ili waendelee na kazi zao hata mbele ya matatizo yaliyosababishwa na janga la dharura ya kiafya ya virusi vya corona.
Kwa upande wao Papa Francisko anatazama hasa wale wote wanaouza magazeti barabarani na ambao sehemu kubwa ni wale wasio kuwa na kazi maalum, watu ambao mara nyingi wamewekwa pembezoni,na hawana ajira. Mamilioni ya watu hawa ulimwenguni kote wanaishi na wana kazi shukrani ya kuunza magazeti haya maalum.
Huu ni ukweli anaelezea Papa, ulioundwa na magazeti zaidi ya 100 ya barabarani ulimwenguni kote, yaliyochapishwa katika nchi 35 tofauti na kwa lugha 25 tofauti, lakini zaidi ya yote yanatoa mapato kwa zaidi ya watu 20,500 wasio na makazi. Nchini Italia, Papa anakumbusha kuwa, kuna uzoefu mzuri wa Scarp de ‘ tenis ,yaani ambao ni mradi wa Caritas unaoruhusu watu zaidi ya 130 wenye shida ili kupata mapato na kwa njia hiyo umewezesha kupata haki msingi za uraia.
Virusi vya corona, vimepigisha magoti hali halisi na ambayo Papa Francisko anaonesha ukaribu wake, lakini pia kwa kuwatia moyo kwa wakati ujao na roho ya urafiki kwa sababu kazi wanayoifanya pia inafafanua historia ya matumaini. Papa Francisko anahimisha barua yake kwa kuwatia moyo kwamba “Janga limefanya kazi yenu kuwa ngumu lakini nina uhakika kuwa mtandao mkubwa wa magazeti ya barabarani duniani utarudi kuwa wenye nguvu zaidi ya awali”. Aidha: “Kutazama masikini zaidi katika siku hizi, inawezekana kusaidia sisi sote kuwa na dhamiri ya kile ambacho kwa hakika kimetutokea na katika hali yetu halisi”. Kwa ninyi nyote ninawatumia ujumbe wa kuwatia moyo na wa urafiki kidugu”.