Wizara ya Afya Zanzibar, leo Aprili 19, 2020 imetangaza ongezeko la wagonjwa 23 wapya wa Corona na kufanya idadi ya wagonjwa kufikia 58 kutoka 35, kati ya wagonjwa wapya, 21 ni raia wa Tanzania, wawili raia wa kigeni (Mfaransa na raia wa Cuba), wagonjwa wawili wapya wamefariki.

 

Baada ya Wizara ya Afya Zanzibar kutangaza ongezeko la wagonjwa 23 wapya wa Corona na kufanya wafikie 58, sasa jumla ya maambukizi Tanzania inafikia 170 kutoka 147 huku ongezeko la vifo viwili Zanzibar likifanya vifo Tanzania nzima vifikie saba kutoka vifo vitano.