Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Machi 18, 2020 ametangaza ongezeko la wagonjwa wawili wa virusi vya corona Tanzania mmoja amekutwa Zanzibar na mmoja Dar es Salaam wote ni raia wa kigeni. Jumla wamefikia watatu.
“Shughuli za masoko na maduka zitaendelea kama kawaida ila tunaomba msisitizo zaidi kuwasihi Wananchi kuepuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima. Vyombo vya usafirishaji tunawasihi watu kuwa level seat na kupunguza misongamano.” amesema Waziri Mkuu – Kassimu Majaliwa