Wamisionari wakiwa Nje kabla ya kuonana na Baba Askofu Mkuu

Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni Jimbo kuu Katoliki la Dodoma tumemtembelea Mha. Baba Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya O.F.M Cap.

Leo siku ya Tarehe 11/03/2020 Wamisionari Jimbo Kuu la Dodoma tulipata nafasi ya kwenda kuonana  na Baba Askofu  na tulipata Fursa ya kumshirikisha juu ya Utume wetu pia kuhusu Annivesary yetu ya Miaka 10, na mambo mengine yanayohusu uinjilishaji wa wamisionari Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma,

Askofu alifurahi sana kuujua utume wetu juu ya hasa nini tunakifanya na namna gani tunaendesha utume huu,na ametupokea vizuri kabisa.

Pamoja na hayo tulimkabidhi katekisimu 50 kwa lengo la uinjilishaji na amezipokea kwa Moyo mkunjufu,pamoja na T-Shirt ya Umoja wetu.

Pia Baba Askofu ameahidi kushiriki nasi katika Misa ya Ufunguzi ya Annivesary yetu na ameshaandika kwenye diary yake. Hivyo hima Wamisionari tujipange kuja Dodoma,utume kwetu umepamba moto. Na maandalizi yamekwishaanza karibuni sana.