RAIS  John  Magufuli  na mkewe, Janeth Magufuli, leo Februari 26, 2020, wameshiriki Misa ya Jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oyster Bay  jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipakwa majivu na Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Padre Dkt. Alister Makubi wakati wa Ibada ya Jumatano ya Majivu jijini Dar es salaam leo Februari 26, 2020.
Mama Janeth Magufuli, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipakwa majivu na Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Padre Dkt. Alister Makubi wakati wa Ibada ya Jumatano ya Majivu jijini Dar es salaam leo Februari 26, 2020