Kiongozi mstaafu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict, wa 16 amepinga pendekezo la mrithi wake, Papa Francis, kuwaruhusu wanaume waliooa kuwa makasisi katika eneo la Amazon.

Papa Benedict amesema utaratibu wa kutooa huwasaidia makasisi kuangazia majukumu yao zaidi.

Mwezi Juni mwaka 2019 Papa Francis alitoa wito kuhusu wazo la kuwafanya wanaume waliooa kuwa makasisi katika maeneo yanayozunguka mto Amazon, Amerika ya Kusini.