KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis,  ameomba msamaha kwa kitendo chake cha kumpiga mmoja wa waumini wa kanisa hilo Desemba 31 mwaka 2019, akiwa Vatican.

Papa alionesha kushindwa kuvumilia baada ya kuvutwa mkono na muumini huyo, nakuamua kumpiga baada ya kughadhibika.

Kiongozi huyo wa kidini alikuwa akisalimiana na watoto na mahujaji huku akiinga eneo la Kanisa la Nativity jijini Vatican ambapo mwanamke mmoja aliyekuwa anasubiri salamu alimvuta mkono baada ya kumuona akiondoka bila kumsalimu na hapo ndipo papa alipogeuka na kumpiga makofi mara kadhaa mkononi huku akijaribu kujinasua.

Katika misa aliyoifanya Januari mosi, mwaka huu ameomba radhi kwa kuwa mfano mbaya kwa watu, kwa kukosa uvumilivu na kukasirika.