PAPA FRANCIS wa leo (Jumanne) anaadhimisha mwaka wa 83 wa kuzaliwa kwake. Wiki iliyopita aliadhimisha mwaka wa 50 wa upadrisho wake.

Ujumbe mbalimbali wa kumtakia heri katika tukio hilo umekuwa ukimiminika kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Mwaka jana Papa aliadhimisha siku ya kuzaliwa kwake kwa kufanya karamu ndogo na kundi la watoto wadogo waliokuwa wakipatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Santa Marta kilichoko Vatican.

Jina halisi la Papa ni Jorge Mario Bergoglio, aliyezaliwa jijini Buenos Aires, Argentina, Desemba 17, 1936, akiwa mtoto wa wahamiaji kutoka Italia. Mwaka 1958 alijiunga na kundi la Jesuit Order ambapo mwaka 1998 aliteuliwa na Papa John Paul wa Pili kuwa Askofu Mkuu wa Buenos Aires.

Papa Francis ambaye alichaguliwa kushika nafasi hiyo Machi 13, 2013, ni papa wa 266 wa Kanisa Katoliki.