Siku ya Tarehe 08.12.2019 Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni walisali katika Kanisa la Kiaskofu Jimboni Same na Baba Askofu Rogath Kimario na Kuwashukuru Wamisionari wakatiliki Mtandaoni kwa Ujio wao na Hakika amekili wamisionari wanafanya kazi nzuri na ya kipekee.

 

Baba Askofu Rogath Kimario Aliwaasa wamisionari kutikata tamaa maana kazi yao nzuri Mwenyezi Mungu Ataibariki mno. Na kuwaomba wana Same Kujiunga na wamisionari wakatoliki mtandaoni kwa vile kundi hili ni mfano wa kuigwa.

Baada ya Misa Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni wakiwa katika picha ya pamoja na Baba Askofu Rogath Kimario.
Shughuli ya ziara hiyo ilihitimishwa kwa Baba Askofu Rogath Kimario Kuwapeleka wamisionari waliobaki baada ya wengine kuanza kuondoka kutokana na umbali wa walikotoka, kwenye Kanisa jipya jimboni hapo na kuwaomba wamisionari wakatoliki mtandaoni kumsaidia kwa chochote ili kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo. Wamisionari walifanya harambee ya haraka na kuoata ahadi ya Tsh 3,000,000 na na Cash 160,000 wamisionari wameahidi kuendelea kukusanya chochote watakachopata na kukabidhi kwake ifikapo mwezi Februari 2020.