Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni Desemba 7, 2019 tulifanyanya Matendo ya Huruma kwa kukabidhi mahitaji mbalimbali katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Mama Kevina kilichopo Jimbo Katoliki la Same, mkoa wa Kilimanjaro ambapo baadhi ya Wamisionari kutoka majimbo mbalimbali ya Tanzania walianza kuwasili katika jimbo la Same kuanzia Tarehe 06.12.2019 na kufanya manunuzi ya mahitaji ya watoto hao Tarehe 6.12.2019 hiyo hiyo. Wamisiinari walikabidhi majitoleo yao mnamo tarehe 7.12.2019.
Wamisionari Wakatoliki walikabidhi mahitaji yafuatayo katika kituo hicho ni pamoja na
1.Sukari
2.Mchele
3.Maharage
4.Mafuta ya kupikia
5.Sabuni za unga
6.Vifaranga vya kuku
7.Chakula cha kuku
8.Taulo za kike
9.Wamenunua pia sale walizovaa watoto siku hiyo
10.Kufanya Service uzio wa eneo la shule kwa kupaka Rangi na kurudishia maandishi.
Hivi na vingine vingi ndio majitoleo Yaliyopelekwa ikiwemo pamoja na kukabidhi cash 1,000,000/= Milioni moja Taslim.
Â