Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu mkuu Novatus Rugambwa kuwa Balozi mpya wa Vatican kwenye Visiwa vya Marshall, Kiribati, Nauru na Tonga. Kabla ya uteuzi huu Askofu Mkuu Rugambwa alikuwa Balozi wa Vatican nchini New Zealand, Fiji, Palau na Mwakilishi wa Kitume kwenye Bahari ya Pacific, na ataendelea pia wadhifa huo huo.
Itakumbukwa kwamba, Askofu Mkuu Novatus Rugambwa alizaliwa tarehe 8 Oktoba 1957, Katika Jimbo Katoliki la Bukoba nchini Tanzania. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre mikononi mwa Askofu Nestorius Timanywa kunako tarehe 6 Julai 1986. Akajiunga na utume wa kidiplomasia mjini Vatican hapo tarehe 1 Julai 1991.
Baada ya kufanya kazi mbali mbali katika Balozi za Vatican, kunako tarehe 28 Juni 2007 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto wa XVI akamteuwa kuwa Katibu mkuu msaidizi wa Baraza la Kipapa la shughuli za kichungaji kwa ajili ya wakimbizi na watu wasiokuwa na makazi maalum.
Kwa namna ya pekee tunaalikwa kumuombea Baba yetu Askofu Mkuu Rugambwa ili Mwenyezi Mungu aendelee kumuongoza katika Utume wake