MWANZO: Zab. 25:1-3 Ee Bwana, nakuinulia nafsi yangu, Ee Mungu wangu, nimekutumaini wewe, nisiaibike, adui zangu wasifurahi kwa kunishinda. Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja.
SOMO 1.
Isa. 2: 1-5
Hili ni neno aliloliona Isaya mwana wa Amozi katika habari za Yuda na Yerusalemu. Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu. Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. Enyi wa nyumba ya Israeli, njioni, twende katika nuru ya Bwana.
Neno La Bwana…….Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI:
Zab 122:1-5
(K)Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana.
Nalifurahi waliponiambia,
na twende nyumbani kwa Bwana.
Miguu yetu imesimama, ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu. (R)
Ee Yerusalemu uliyejengwa kama mji ulioshikamana,
huko ndiko waliko-panda kabila,
kabila za Bwana. (R)
Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu,
nisema sasa, Amani ikae nawe. Kwa ajili ya nyumba ya Bwana,
Mungu wetu, nikutafutie mema. (R)
SOMO 2
Rum.13: 11-14
Ndugu zangu, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini. Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia; basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake.
Neno La Bwana……..Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO.
Zaburi 55:5
Aleluya, Aleluya,
Ee Bwana utuonyeshe rehema zako, utupe na wokovu wako.
Aleluya!
INJILI
Mt. 23: 35-43
Siku ile, Yesu aliwaambia wafuasi wake kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakio na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa; wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa. Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.
Neno la Bwana………..Sifa kwako ee Kristo.
Jumapili, December 1, 2019.Dominika ya 1 ya Majilio. Mwaka “A” wa KanisaIsa 2:1-5
Zab 121:1-2, 4-9
Rum 13:11-14
Mt 24: 37-44
MOYO ULIO MAKINI!!
Kipindi cha majilio kimeanza! Jumapili ya kwanza ya majilio inaashiria mwanzo wa mwaka mpya wa liturujia, safari mpya katika maisha ya kanisa takatifu Katoliki. Kwahiyo kanisa linatualika tujiunge na “safari hii ya Imani” . Kipindi cha majilio kina tuandaa kwa sherehe ya Kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Kilitrujia ni kipindi cha adhimisho la tukio lililopita, historia ya kuzaliwa Bwana wetu Yesu Kristo. Kuzaliwa kwa Kristo kama Mwanadamu kumeshatokea. Maandalizi yetu sio kama yale ya Waisraeli wanao subiria wakati ujao, bali sisi kama Waisraeli wapya tunaoishi wakati wetu tukijua ujio wa Bwana wakati wetu.
Embu jaribu kufikiria, mara moja unaamka asubuhi unakuta ni siku ya Noeli hasubuhi na hukujiandaa kwa chochote? Huna nguo yeyote, hajanunua chakula, na hujapanga mpango wowote. Kwa hakika huwezi kuruhusu kitu kama hicho kitokee, lakini ajabu tunaruhusu hali kama hiyo itokee katika roho zetu. Mara nyingi hatujiandai kusherekea vizuri kuzaliwa kwa Yesu katika mioyo yetu. Kipindi cha Majilio ni kipindi cha kujiandaa kumkaribisha tena Yesu ndani ya mioyo yetu.
Je, leo Litrujia ya neno inatuambia nini leo?
Maandalizi yetu yana aina mbili, kwanza kabisa tunaitwa kuharibu silaha za vita nakuvifanya kuwa vifaa vya kulimia na wala tusiwaandae askari kwa ajili ya vita (somo la kwanza). Tunapaswa tujifunze kuweka mbali matendo ya giza, ulevi, ufisadi, uasherati, magomvi, malumbano, na wivu na mengine mengi.
Katika hali nyingine, japo tunapaswa kujiingiza katika shughuli zetu za kila siku na majukumu, hatupaswi kuishi kama vile hakuna kitu kingine zaidi ya shughuli zetu na majukumu yetu. Mara ngingi kwa ujumla tuna mahangaiko na mambo mengi. Tunapaswa kuwa na muda maalumu uliotengwa kwa ajili ya uhusiano wetu na urafiki wetu na Mungu. Na hivyo kuwa wakati mwingine kutenga muda fulani katika siku kuwa kwa ajili ya Mung tu. Tuna alikwa kwenda katika nyua za Bwana au kupanda mlima wa Bwana. Mlima ni alama ya uwepo wa Mungu. Ni Yerusalemu ya Mbinguni. Ni wito wa kuunganika na Mungu. Kupanda mlima si tu kuwa mbali na uovu na dhambi, bali ni kuwa Mtakatifu. Kwa maneno ya Paulo ni “kumvaa Kristo”. Ni kuwa na roho na hali ya Yesu Kristo.
Tutafanyaje haya?
Ni kwa kuwa na moyo wa unyenyekevu ulio makini. Mchezaji mzuri wa mpira ni yule aliyeweka mawazo yake katika ule mpira na wachezaji wenzake. Mwanafunzi mzuri ni yule anayeweka mawazo yake darasani na kusikiliza anacho fundisha mwalimu. Mkatoliki mzuri ni yule aliyeweka mawazo yake ya roho na mwili kumwelekea Mungu, akijiingiza kwenye sala daima na kufanya matendo ya huruma. Tunatambua kuwa Noeli itakuja tarehe 25, mwezi wa 12. Tutakuwa tunaimba nyimbo mbali mbali, kanisa na mazingira yetu yatapambwa vizuri na nyota na maua mbali mbali, watu watanunua nguo mpya. Yote haya ni mazuri. Lakini uwepo wa Kristo tusiuchukulie katika hali hii tu. Yeye anakuja katika hali ya ukimya wa roho zetu ili tuweze kukuwa naye katika mioyo yetu! Tunapaswa kujiandaa kwa kuungama dhambi zetu vizuri na kutakasa roho zetu. Lakini pia lazima kutambua kuungama tu ya zamani sio alama ya kukuwa na kuwa na hali njema. Tunapaswa kukuwa katika upendo na Mungu. Kama vile kuzaliwa kwa Yesu, Mungu alikuwa karibu kabisa na ubinadamu, tunapaswa kukuwa katika utakatifu na tunapaswa kukutana na Yesu. Kukuwa katika utakatifu maana yake kujifunza jinsi ya kuboresha uhusiano wetu na Mungu kwa sala alisema Mt. Yohane Paulo II.
Tunapaswa kuwa waangalifu na pia kuwa washiriki katika maisha ya sakramenti katika Kanisa. Tunapaswa tuadhimishe Ekaristi katika hali inayofaa, kwani “Kila wakati Kanisa linavyo adhimisha Ekaristi linakumbuka ahadi yake na kujikita katika yeye “ambaye atakuja”. Katika sala zake linaita ujio wake. “Maranatha!” “njoo Bwana Yesu” Bwana tunaomba neema zako zije na ulimwengu utapita. (Katakisimu ya Kanisa katoliki – 1403).Tamaa yetu ya kuwa karibu na Yesu inatupasa sisi kuwa karibu na ndugu zetu, kwani hakuna kitu kizuri machoni
pa Mungu kama kuwaonea na kuwaonesha huruma ya kweli ndugu zetu. Kwa hali hii halisi, huruma huwa katika hali ya uhalisia katika matendo. Hatupaswi tu kukaa mbele ya Mungu, lakini kukaa kwetu karibu na Mungu ibadilishe maisha yetu, na maisha ya ndugu zetu, na zaidi sana wale wagonjwa, maskini, na wanaoteseka. Tunaomba neema za majilio, zitusaidie kumkaribisha Yesu tukiwa na mioyo iliotayari , makini na minyenyekevu.
Sala: Bwana, kwa jinsi majilio ilivyo anza, nisaidie niweze kuelekeza macho yangu kwako. Nisaidie niweze kufungua masikio yangu kusikia sauti yako. Nisaidie niweze kufungua moyo wangu kwa uwepo wako mtukufu. Ninaomba niwe makini katika hali zote unazotaka kuja kwangu, nina kuamini wewe tu. Amina.
*NB: Ukihitaji shajara ya “ASALI MUBASHARA” ya mwaka 2020 yenye masomo ya kila siku na tafakari zake za Asali Mubashara mwaka mzima wasiliana nami kwa number hizi 0755444471 au 0714002466. Shajara imeshiba na masomo mpaka na zaburi zimechambuliwa kuongeza ufahamu wa maandiko na kukuza hekima yetu kwa Mungu.* *Ukiipata utaipenda mwenyewe, itakusaidia mnoo*