Novena ya kuwaombea marehemu toharani siku ya tatu

Teso kuu la roho maskini ni kuonekana wazi dhambi zao walizotenda na zinazowatisha. Kwa hizo sasa wanateseka katika hali ya kutakaswa. Katika ulimwengu huu, mtu haelewi vyakutosha ubaya na sura ya dhambi, lakini kila kitu kitakuwa dhahiri katika ulimwengu mwingine ujao.

Baba wa milele, Mungu Mtakatifu, Mtakatifu Mwenyezi, Mtakatifu uishie milele, ninakupenda zaidi ya kitu chochote kile, kwa kuwa Wewe ni wema wa milele na ninasikitika kwa moyo wangu wote kwani nilikuumiza Wewe. Nijalie neema zako Ee Mungu wangu, unihurumie mimi na uwahurumie roho maskini wanaoteseka toharani kule mahali pa utakaso.
Baba yetu….
Salamu Maria…
Ee Bwana uwajalie pumziko la milele; Na mwanga wa milele uwaangazie; wapumzike kwa amani. Amina.