Kanuni na Taratibu Mbalimbali.. Kanuni za Uendeshaji wa Kundi
Kanuni za Uendeshaji Vikundi kwenye Mitandao ya Kijamii
a) Kuzingatia sheria ya nchi inayoongoza shughuli za mitandao
b) Kuzingatia sheria, taratibu na Imani ya Kanisa Katoliki
c) Kutojihusisha na shughuli ambazo sio lengo la Kundi kama siasa, nk.
d) Kutojihusisha na uchochezi wa aina yoyote utakaovunja amani

Sifa za Wakatoliki Wanaoweza kuwa Wanachama
a) Awe na utambulisho wa ushiriki wake katika shughuli za kanisa, kwa maana ya Jumuiya, Parokia na Jimbo analosali na kutoa/kupata huduma
b) Awe tayari kukubali kujifunza na kufundisha wengine.
c) Awe tayari kuilinda na kuitetea Imani ya Kanisa Katoliki bila kuionea haya.
d) Awe tayari kushiriki mijadala, michango,na shughuli mbali mbali zitakazo endeshwa na kundi.
e) Awe tayari kujitoa kwa ajili ya shughuli za kundi na kanisa
f) Awe mwaminifu na mwenye tabia njema.

2. Kanuni za Uongozi
Sifa za Wakatoliki Wanaoweza kuwa Viongozi wa Kundi
a) Awe ni Mkatoliki mwenye sakramenti za kanisa
b) Awe anajua kusoma na kuandika vizuri (angalau amehitimu kidato cha nne)
c) Awe anaweza kutumia mitandao ya kijamii.
d) Anaejitambua na kujiheshimu.
e) Mshiriki mzuri kwenye mijadala,na shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na Kundi.
f) Awe na moyo wa kujituma na uwajibikaji kwa ajili ya kundi na Kanisa Katoliki kwa vitendo.
g) Awe mwenye Busara, Hekima, Heshima, Utu, Utii, na Utashi.
h) Awe na uwezo wa kutatua matatizo na migongano itakayojitokeza katika Kundi.
i) Awe mwenye uwezo wa kuhamasisha Shughuli Zitakazoendeshwa na kundi.
j) Awe mwaminifu.

2.2. Miiko ya Uongozi.
a) Kulinda na kuheshimu maamuzi yatayoamuliwa kwenye vikao vya viongozi
b) Kutotoa siri za Vikao Vya uongozi isipokuwa kwa ruhusa maalumu
c) Kutambua mipaka ya utawala
d) Ugomvi matusi na lugha zisizo na busara hazitaruhusiwa.
e) Kiongozi anatakiwa kuwa chachu ya maendeleo ya kundi na kanisa na sio mchochezi.

2.3 Taratibu za Kupata Viongozi
a) Uchaguzi wa viongozi wakuu utafanyika kila baada ya miaka mitatu
b) Majina ya wanaowania uongozi yatapendekezwa na wanachama hai kupitia mitandao ya kijamii inayotumika na kundi baada ya kutolewa kwa tangazo la uchaguzi.
c) Viongozi watachaguliwa kwa kura ya siri katika Mkutano Maalum utakaowakutanisha wanachama wote. Wanachama watakaoshindwa kuhudhuria mkutano maalum wa uchaguzi watapiga kura zao kwa njia ya mtandao.
d) Viongozi watakaochaguliwa kwa kupigiwa kura ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti.
e) Kwa ngazi za kiutendaji kama Katibu na Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, na Msemaji Mkuu wa kundi, Wasimamizi wa Shughuli za Mitandaoni (Admins) na viongozi wa kamati mbalimbali, viongozi watapatikana kwa kuteuliwa kutokana na sifa zao.
d) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Katibu Msaidizi, Mwekahazina na Msemaji Mkuu, Mwenyekiti wa kamati ya mtandao pamoja na Wenyeviti wa Kamati Mbalimbali wataunda Kamati Tendaji ya Kundi.
e) Kamati kuu, pamoja na wenyeviti wa kamati zote na wenyeviti wa majimbo wataunda halmashauri kuu.