Kamati ya Kuratibu Matendo ya Huruma
Kamati hii itawajibika kuratibu zoezi zima la kusaidia wahitaji mara mbili kila mwaka kipindi cha kwaresma na kipindi cha majilio. Kazi ya kamati hii pamoja na mambo mengine ni;
- Kutafuta maeneo yenye mahitaji popote pale Tanzania na kufahamu mahitaji katika eneo husika
- Kusimamia uchangiaji kwa ajili ya kufanikisha matendo ya huruma
- Kuhamasisha michango kutoka kwa wanachama na wasio wanachama
- Kuratibu safari za matendo ya huruma
Kamati itafanya kazi kwa karibu na Uongozi Mkuu au kamati ndogo itakayoteuliwa au Mwanachama Mwakilishi kwenye Jimbo au Parokia ambayo tukio litaenda kufanyika.
Wafuatao wanapendekezwa kuunda kamati hii
- Alfred Lupogo…………. Mwenyekiti
- Angella Assenga………. Katibu
- Veritasi Nderumaki….. Mjumbe
- Salome Ng’ingo……… Mjumbe
- Hellena Chitukuro……. Mjumbe
- Salvina Kyaduma…….. Mjumbe
Kamati hii itasimamiwa na Mweka hazina.