ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo, ameng’atuka wadhifa huo na nafasi yake imechukuliwa na Askofu Mkuu Mwandamizi, Yuda Thaddeus Ruwa’ichi, wa Jimbo kuu la Dar es Salaam.

Hivi karibuni, Askofu Pengo aliomba kupumzika nafasi hiyo ambapo Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francis ameridhia ombi hilo na kumruhusu kupumzika.