PICHA MBALIMBALI ZA MATUKIO YA MATENDO YA HURUMA MBEYA

Pamoja na hayo uongozi wa wamisionari walikabidhi baadhi ya Zawadi kwa

1.Mhashamu Baba Askofu
2.Zawadi za wakuu wa Gereza
3.Zawadi kwa baadhi ya Mapadre wa Jimbo kuu Katoliki la Mbeya.

Katika Safari hii Tulipewa baraka zote na Mhashamu Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya. Askofu Gervas Nyaisonga. Na kuwashukuru na kuwapongeza Wamisionari wakatoliki Mtandaoni kwa namna wanavyofanya kazi yao ya kueneza Neno La Mungu Kupitia Mitandao ya Kijamii. Na kuwaomba wamisionari miaka miwili ijayo kutakuwa na Jubilei yake ya Miaka 25 ya toka apate daraja la upadre. Angefurahi sana kama tutashiriki jubilei hiyo.

Mengine yalivyofanywa na wamisionari wakatoliki mtandaoni ni Kihudhuria misa Takatifu ya Jubeli ya Mapadre wawili waliokuwa wanatimiza miaka 25 ya upadrisho wao katika Kanisa La Kiaskofu la Jimbo kuu katoliki la Mbeya.

Na kuhitimisha Shughuli hiyo Siku ya Jumapili Tarehe 9/06/2019

Kwa Kuhudhuria Adhimisho la Misa Takatifu Ya Pentekosti katika *PAROKIA ROHO MTAKATIFU – RUANDA

Iliyoadhimishwa na Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga.

Na pia Kuwapa nafasi Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni ya Kujitambulisha na kuuelezea kwa kina umisionari huo na Shughuli Zinazofanywa na WAMISIONARI WAKATOLIKI MTANDAONI.

Matukio mbalimbali ya Matendo ya huruma yaliyofanyika katika gereza la Mbozi-Mbeya

       

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *