Historia Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni

Kundi la Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni (Zamani tulijulikana kama Vijana Wakatoliki Tanzania) lilianzishwa mwaka 2010 baada ya Kongamano la Vijana lililofanyika Arusha. Viongozi wa Viwawa Parokia ya Njiro, Arusha ndio waliopata wazo hili la kuunganisha Vijana wote Wakatoliki wa Tanzania kupitia mtandao wa Facebook. Wakatoliki wote na hasa vijana wanapokelewa kujiunga na kundi. Kundi letu halifungamani na Chama chochote cha Kitume wala Jimbo lolote. Ni Mtandao ulioenea Tanzania nzima.Tuna malengo mapana ya kufikisha utume wetu nje ya Tanzania pia. Hadi sasa Kikundi kina wanachama wapatao zaidi ya 10,000 kwenye Facebook. Tunatumia pia mitandao mingine ya Instagram na Whatsapp kuinjilisha.

Kati ya mambo ya msingi yanayofanywa ndani ya kundi ni Elimu juu ya Imani Katoliki kupitia mitandao. Kundi limekuwa msaada mkubwa kwa Wakatoliki wanaohitaji kuelimishwa juu ya jambo lolote ama changamoto yoyote kwenye imani Katoliki. Mashemasi na Mapadre walioko kwenye kundi wamekuwa msaada mkubwa kwa kujibu maswali mengi kwa ufasaha. Tunaamini tumetoa mchango mkubwa katika kuwasaidia Wakatoliki kuielewa imani yao kupitia mitandao.


Toka tumeanza utaratibu huu mwaka 2012, tumeshafanya Matendo ya Huruma kwenye vituo
vifuatavyo;

 • Kituo cha Watoto Yatima cha Mburahati Charity Centre, Jimbo Kuu Katoliki, Dar
 • es Salaam (Januari 2012)
 • Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Dar es Salaam (Mei 2012)
 • Kituo cha Kulelea watoto Yatima cha Camp Joshua, Arusha (Januari 2013)
 • Kituo cha Kulelea Watoto walemavu na wenye Mtindio wa Ubongo cha Amani, Jimbo Katoliki la Morogoro (Aprili 2013)
 • Kituo cha watoto walemavu wa akili cha Miyuji Cheshire Home, Jimbo Katoliki la Dodoma (Januari 2014)
 • Kituo cha watoto yatima cha Nyumba ya Furaha (Cassa dell Gioia), Jimbo Katoliki la Tanga (June 2014)
 • Watoto Wagonjwa wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam (December 2014)
 • Kituo cha Kulea Wazee cha Welezo, Jimbo Katoliki Zanzibar (Aprili 2015)
 • Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Karibu Nyumbani, Kibaha, Jimbo Katoliki la Dar es Salaam (Januari 2016)
 • Kituo cha Kulea Watoto wenye Mtindio wa Ubongo cha Bethlehem Centre, Jimbo Katoliki la Ifakara (Aprili 2016)
 • Kuchangia Ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Katembo, Ikwiriri, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam (Februari 2017)
 • Kuchangia Uchimbaji na Ujenzi wa Kisima cha Maji Safi kwenye Mahabusu ya Watoto Upanga Dar es Salaam (June 2017)